October 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

PORTO, PORTUGAL - FEBRUARY 27: Kai Havertz of Leverkusen during the UEFA Europa League round of 32 second leg match between FC Porto and Bayer 04 Leverkusen at Estadio do Dragao on February 27, 2020 in Porto, Portugal. (Photo by Jörg Schüler/Getty Images)

Tetesi za soka leo Alhamisi Julai 9, 2020 Barani Ulaya

Manchester City, Juventus na Barcelona zinapigana vikumbo kuwania saini ya winga wa Wolves Adama Traore mwenye umri wa miaka 24 raia wa Uhispania (ESPN).

Klabu ya Chelsea wanapigiwa upatu kumsajili mshambuliaji wa Bayer Leverkusen Kai Havertz, mwenye umri wa mika 21, baada ya klabu kadhaa za Ujerumani kushindwa kufikia bei ya euro milioni 90 kumpata mchezaji huyo. (Goal).

Barcelona imeuangazia usajili wa kiungo wa kati wa Tottenham Tanguy Ndombele, mwenye umri wa miaka 23 raia wa Ufaransa na mlinzi Ryan Sessegnon kutoka Uingereza katika mpango utakaohusisha ubadilishanaji wa wachezaji. (Evening Standard).

Klabu ya Tottenham Spurs huwenda ikamsajili kwa mkopo Sessegnon msimu huu wa joto licha ya hofu kwamba nyota ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20, inafifia chini ya ukufunzi wa kocha Jose Mourinho. (Telegraph).

Dortmund imeipatia Manchester United hadi Agosti 10 mwaka huu kukamilisha usajiliwa wa winga wao Tammy Abraham, mwenye umri wa miaka 22 raia wa England huku Jadon
Sancho ameiambia Chelsea kwamba anataka mkataba mpya wa thamani ya pauni 130,000 kwa wiki. (Times).

Kocha wa West Ham David Moyes anatafakari uwezekano wa kuwanunua wachezaji wa Manchester United Phil Jones, mwenye umri wa miaka 28, na Jesse Lingard mwenye umri wa miaka27. (Independent).

Arsenal, West Ham na Everton wapo kwenye vita kali ya kuwania saini ya beki wa Athletic Bilbao na Uhispania Unai Nunez, mwenye umri wa miaka 23. (AS, via Sport Witness).

Rais wa Barcelona Josep Bartomeu amesema klabu hiyo huenda isimsajili tena mshambuliaji wa Brazil Neymar, mwenye umri wa miaka 28, kutoka Paris St-Germain msimu huu wa joto. (RAC1 – in Spanish).

Saint-Etienne ina matumaini ya kumhifadhi kwa mkopo beki wa Arsenal Mfaransa William Saliba, mwenye umri wa miaka 19.

Winga wa Uholanzi Tahith Chong, 20, huenda akaondoka Manchester United kwa mkopo msimu ujao, kwa mujibu wa ajenti wake. (Stretty News).

Barcelona imemhakikishia mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, mwenye umri wa miaka 29, kuwa yupo kwenye mpango wa klabu hiyo msimu ujao. (L’Equipe – in French)

%%%%%%%%%%%%