December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Uvumbuzi Wanawake, Wasichana katika Sayansi – SBL

Baadhi ya wahitimu wa programu ya SBL Glory Grace Mpinga (kushoto),Sanura Adam(kati) na Glory Hungu (kulia) wakiwa kiwanda cha SBL Moshi ambapo kwa Sasa wameajiriwa na kampuni hiyo.

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online

JUKUMU la wanawake katika nyanja ya uvumbuzi wa kisayansi na uendelevu limekuwa la lazima katika kuchochea kusonga mbele na kutengeneza upya mazingira ya utafiti na maendeleo. Licha ya juhudi zao zote, uwakilishi wa wanawake unafikia asilimia 33.3 ya watafiti duniani kote, hata hivyo kazi zao bado hazipati heshima inayostahili [UNESCO: Ripoti ya Sayansi: kuelekea 2030 (2021)].

Rispa Hatibu, Meneja wa Mawasiliano na Uendelevu wa kampuni ya Serengeti Breweries Limited, amethibitisha namna ambavyo kampuni kwa miaka mingi imekuwa ikiliadhimisha hili, siku zote ikiongoza katika juhudi na mafanikio ya kipekee ya wanawake na wasichana katika sayansi na kufanya juhudi zao ziwe endelevu.

Wanawake wana mchango upi katika Utafiti wa Kisayansi, Ubunifu, na Uendelevu?

Hapa SBL, tunajivunia safu yetu ya Spirit Cube ambayo inaongozwa na wanawake pekee, imekuwa mwanga kwa ubunifu, uendelevu, na ujumuishi katika nyanja ya utafiti wa kisayansi. Wanawake katika SBL wamechangia kwa kiasi kikubwa katika maeneo mbalimbali, kuanzia kuongoza maendeleo ya kiteknolojia ya nishati mbadala mpaka uongozi katika utafiti wa vifaa endelevu.

Kwa kuongezea, kujitolea kwa timu yetu katika kuvuka mipaka zaidi ya ubunifu huku tukidumisha kanuni za utunzaji wa mazingira na utofauti umepelekea maendeleo ya bidhaa za kisasa ambazo si tu zinakidhi viwango vya juu vya ubora bali pia inaashiria dhamira yetu ya kujenga mustakabali endelevu na wenye ujumuishi kwa wote.

Je, unaweza kutushirikisha simulizi za viongozi wanawake ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa katika sayansi na uendelevu ndani ya SBL?

Ndani ya familia ya SBL, kuna viongozi wanawake wa aina yake katika idara za ugavi na rasilimali watu wenye mchango mkubwa katika kufanikisha dhamira yetu ya sayansi na uendelevu.

Chukulia, Natalia Kimacha, Meneja wa Uzalishaji Bora wa SBL na Saraphine Mwamaso, Meneja wa Mabadiliko ya Chapa wa SBL ambaye anaongoza programu yetu ya mafunzo ya STEM (masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati) kwa vijana. Kupitia miongozo yao, wanawake vijana wengi wamewezeshwa kufuatilia masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi, na hisabati. Wanafunzi hawa wamefanikiwa, wakileta mitazamo mipya na suluhisho za ubunifu kwa miradi yetu.

Kwa mfano, Evelyne, mmoja wa wanafunzi wetu wa STEM, alitengeneza suluhisho la vifungashio linalohifadhi mazingira kwa kiasi kikubwa huku tukiendelea kudumisha uadilifu kupitia bidhaa zetu. Kujitolea kwa Natalia na Saraphina katika kulea vipaji na kukuza utamaduni wa ujumuishi sio tu kumezalisha nguvukazi yetu bali pia kumepeleka mbele kuelekea mustakabali endelevu zaidi.

SBL ina mchango na malengo gani ya kukuza usawa wa jinsia na utofauti katika uongozi wa kisayansi?

Tuna dhamira ya dhati katika hili kupitia awamu tofauti za programu yetu ya wanafunzi wa STEM ambapo tunalenga kutoa fursa kwa wanawake vijana kuangazia na kung’ara katika fani za STEM, kuondoa vizuizi vya kuingia na kukuza utamaduni wa ushirikishwaji.

Kongamano letu la Wanawake linatumika kama jukwaa la kutetea mwongozo na ukuaji wa taaluma, kuwawezesha wanawake kufikia malengo yao kamili huku wakisaidia jamii zao. Kwa kuwezesha ulezi, kuwakutanisha na watu tofauti, na fursa za kujenga ujuzi, tunajitahidi kutengeneza mazingira ambayo kila mwanamke anajisikia kuthaminiwa, kusaidiwa, na kuhamasishwa kuongoza katika sayansi na zaidi. Lengo letu si tu kukuza nguvukazi yenye utofauti na ujumuishi bali pia kusukuma mbele gurudumu la uvumbuzi na weledi kupitia mitazamo na michango ya kipekee kutoka kwa kila mtu.

Je, sera za SBL za kiungozi, kiutendaji na mazingira ya kazini zinachangiaje katika kuunga mkono maendeleo ya wanawake katika nafasi za uongozi wa kisayansi?

Sera yetu ya mafunzo kwa wahitimu imeweka kipaumbele utofauti na ujumuishi, kuwapatia wanawake fursa ya kupata uzoefu wa vitendo na kuendeleza stadi katika fani za STEM. Kupitia juhudi zetu maalum za kuajiri na programu za ulezi, tunahakikisha wanawake wanapata rasilimali na msaada wanaohitaji ili kufanikiwa ndani ya kampuni yetu.

Zaidi ya hayo, utamaduni wetu wa ujumuishi, ukiongozwa na miongozo ya utofauti, unakuza mazingira ambayo wafanyakazi wote wanajisikia kuthaminiwa na kuwezeshwa kuchangia mitazamo ya kipekee waliyonayo, hivyo kuondoa vizuizi na kutengeneza njia kwa wanawake kung’ara katika uongozi wa kisayansi ndani ya SBL na zaidi.

Kwa mfano, mtandao wetu wa Jukwaa la Wanawake unatumika kama msingi wa maendeleo ya kitaaluma na kukuza ajira za wanawake katika STEM. Unatoa rasilimali nyingi, ikiwemo ulezi, mafunzo, na fursa za ukuaji kibinafsi na kitaaluma.

Kupitia matukio kama haya mara kwa mara, warsha, na semina, wanachama wa mtandao wa Jukwaa la Wanawake wanakutana na wenzao, kubadilishana maarifa na uzoefu, na kupata ufahamu muhimu katika kuendesha taaluma. Kwa kukuza jamii inayotoa msaada na kutoa fursa za ulezi na mafunzo, tumejizatiti kuwajengea wanawake nyenzo na rasilimali wanazohitaji ili kufanikiwa na kusonga mbele katika taaluma zao za STEM ndani ya shirika letu na zaidi.