May 3, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makonda amsadia mwanamama aliyepatwa na janga la kulawitiwa mtoto wake

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mwanamama mkazi wa Iringa amemueleza Mwenezi Makonda changamoto nzito anayoipitia kutokana na mkasa aliyokumbana nao kutoka kwa Dada yake aliyemtendea vibaya mtoto wake wa kiume ambaye kwasasa ana miaka 5.

Mwanamama huyo amesema alikuwa Iringa na baada ya kukosa nafasi ya kuongea ilimpasa kumfata Mwenezi Makonda hadi Njombe ambapo ndipo amepata nafasi hiyo, Katika maelezo yake amesema awali mtoto wake alikuwa mzima wa afya na alipomuacha kwa dada yake akampiga, kamvunja miguu na mikono na kumpasua maeneo ya kichwani pamoja na kulaitiwa vibaya kiasi cha kupelekea kuoza.

Ameendelea kueleza kuwa ametoka Iringa kufuatilia kesi yake huku mtoto akiwa ICU kitengo cha MOI hospitali ya Muhimbili zaidi ya miezi miwili kwa matibabu lakini ana zaidi ya miaka 3 bado haki haijatendeka kwa mtoto wake na ameshindwa kwasababu aliwekwa chini ya ustawi wa jamii.

Baada ya kuendelea kufuatilia zaidi, Mama huyo ameeleza kuwa kupitia ustawi wa jamii walitoa hukumu kwa huyo dada yake ya kumlipa fidia ya Tsh Milioni 2 na kumpa kifungo cha nje cha miaka 3 na kijana wake aliyefanya tukio la kumlawaiti mtoto wake kuonekana hana hatia kwa madai kuwa mule ndani kulikuwa na wavulana wawili.

“Mtoto wangu alikuwa ni mzima wa Afya lakini nilimuachia dada yangu akampiga kichwani, akamvunja miguu, akampasua kichwa pia alilawitiwa sana mpaka alioza, nimetoka iringa kufatilia kesi yangu mtoto akiwa muhimbili ICU pale MOI, nimekaa sana kama miezi miwili, nimefatilia haki yangu ndani ya miaka mitatu lakini wananizungusha nikiwa chini ya ustawi wa jamii ndani ya miaka mitatu na mwaka Jana wametoa Hukumu na kusema kwamba kwasababu mama wa yule mtoto aliyekuwa anamlawiti mtoto wangu ni mtu mzima na alikuwa anashirikiana na mama yake”

“Hakimu amehukumu mwezi wa tatu mwaka jana anasema kwamba mtoto atalipwa fidia ya Milioni 2 na mama aliyechapa mtoto atafungwa miaka mitatu kifungo Cha nje na kijana wake Hana hatia kwasababu mule ndani kulikuwa na wanaume zaidi ya wawili”

Aidha mwanamama huyo ameonesha simanzi kubwa zaidi na kumueleza Mwenezi Makonda kuwa ameishi miaka 3 katika kituo cha watoto yatima akiwa chini ya ustawi wa jamii bila mtoto wake kupata msaada na zile milioni 2 alizokuwa amepewa kama fidia akazitumia kwa kipimo cha CT Scan kupima masikio na macho na hadi hatua aliyofikia mtoto kwasasa ni hawezi kufanya chochote hata kutembea hawezi.

Mwanamama huyo amemuomba Mwenezi Makonda kumsaidia kwakuwa anatakiwa kwenda kliniki katika hospitali ya Muhimbili kila baada ya miezi 3 na hajaenda mwaka mzima katika mwaka wa 2023 kutokana na kukosa fedha ya kukidhi na Bima yake ya Afya imeshakwisha muda wake.

“Nateseka sana nimekaa miaka mitatu kwenye kituo Cha watoto yatima , nikawaomba ustawi wa jamii niondoke , nimekuja mpaka hapa na mtoto bima yake imeisha, na sijapenda kliniki mda mrefu, muhimbili wameshatoa majibu kuwa mtoto hawezi kupona tena na atabaki kuwa tegemezi, naomba mnisaidie Sina pa kukaa wala kushika”

“Mtoto wangu amepoteza dira kabisa, labda angekua Rais au makonda wa kesho” Alisema

Kutokana na hayo yote na kwa kwa upendo na dhamira njema ya Mwenyekiti wa CCM na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mwenezi Makonda amemueleza mama huyo kuwa Chama Cha Mapinduzi kitamsaidia kumpatia Bima ya Afya ya Mama na Mtoto, Kumpatia Kiasi cha Tsh Milioni 5 kumuwezesha katika biashara pamoja na kumsaidia kumfikisha Dar es salaam kwaajili ya kuudhuria kliniki katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Aidha, Mwenezi Makonda alifanya harambee kwa Viongozi wa Chama , Serikali na Wananchi waliodhuria katika mkutano wa hadhara uliofanyika Makambako ambapo aliwezesha kupatikana kwa kiasi kingine cha fedha na kupelekea Mwanamam huyo kupata jumla ya Tsh Milioni 10,007,900/=

” Katika kila nyakati ngumu, yapasa kufahamu kuwa Mungu pamoja nasi…Mama tutakupatia Bima ya Afya kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kesho tutakusaidia kufika Muhimbili Dar es salaam kuendelea na kliniki na tutakupatia mtaji wa Milioni 5 kufanya biashara katika kukusaidia kumhudumia mtoto…Mungu yupo na kikubwa zaidi hao waliofanya hayo tumuachie Mungu na tuendelee kumuombea mtoto wetu ” Alisema Mwenezi Makonda.