Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya
JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)linamshikilia mkazi wa Itiji ,Pius Komba (70) kwa tuhuma za kujihusisha na matukio mbalimbali ya kughushi nyaraka, mihuri bandia kwa kuwapatia wanachama wa mfuko huo ili waweze kupata mafao kinyume cha sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya,Benjamin Kuzaga amesema kuwa mtuhumiwa alikamatwa Januari 25 mwaka huu katika eneo la Retco mkoani hapa wakati jeshi hilo lilipokuwa kwenye msako wa pamoja na maafisa wa mfuko huo katika maeneo mbalimbali mkoani hapa.
“Baada ya msako huu tulifanikiwa kumtia mbaroni kinara wa kuandaa nyaraka na mihuri bandia na kuwapa wanachama wa NSSF ili wapate mafao kinyume na sheria ambayo inayosimamia ulipwaji wa mafao huo”amesema Kamanda Kuzaga.
Hata hivyo Kamanda Kuzaga amesema kuwa mtuhumiwa amekuwa akishirikiana na wanachama wa mfuko na baadhi ya maafisa rasilimali watu wa makampuni wanayofanyia kazi kufanya udanganyifu wa taarifa zinazohitajika ili kulipa mafao kwa mujibi wa sheria ya NSSF sura ya 50 marejeo ya mwaka 2018 kifungu 72 (1) (a) (b).
“Katika msako huo ambao polisi walishirikiana kwa pamoja na kumbaini mtuhumiwa huyo akiwa maeneo ya Retco Mkoani hapa,”amesema.
Akielezea zaidi Kamanda Kuzaga amesema kuwa Siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la vishoka/matapeli ambao wamekuwa wakiandaa nyaraka (barua za kuachishwa kazi) za kughushi ambazo hutengeneza na kuwapa wanachama wa mfuko kwenda kufungua madai kinyume na taratibu ambazo ziko wazi kuwa ili mwanachama apate mafao ni lazima awe ameachishwa kazi na anakidhi vigezo vilivyopo kwa mujibi wa sheria.
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili akiwemo raia wa nchini Rwanda Assouman Gahigiro [48] na Winny Bruno [31] mkazi wa Kiwira Wilaya ya Rungwe kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya aina ya Bhangi kilogramu 20.
Watuhumiwa hao walikamatwa Januari 27, mwaka huu katika kizuizi cha Polisi cha Kayuki kilichopo barabara kuu ya Kyela – Tukuyu ambapo watuhumiwa walikuwa abiria kwenye gari iliyokuwa ikitokea Kyela kuelekea Mbeya Mjini, askari waliokuwepo eneo hilo walilisimamisha gari hilo na kufanya ukaguzi na ndipo walibaini Bhangi iliyokuwa imefichwa kwenye vifungashio vya Nylon na kuwekwa ndani ya begi la nguo.
Hata hivyo Kuzaga amesema Polisi inaendelea na upelelezi kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji ili kubaini uhalali wa mtuhumiwa Assouman Gahigiro kuwepo nchini wakati taratibu nyingine za kumfikisha mahakamani kwa tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya zikiendelea.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi