NA K-VSI BLOG/KHALFAN SAID, ARUSHA
MAADHIMISHO
ya 3 ya Wiki ya Huduma ya Fedha Kitaifa, yamefunguliwa rasmi na Wazri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, katika Uwanja wa Sheikh Amri
Abeid jijini Arusha, Novemba 22, 2023.
Mfuko
wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), ambao uko chini ya Ofisi ya
Waziri Mkuu, ni miongoni mwa taasisi za serikali zinazoshiriki katika
maadhimisho hayo yenye kauli mbiu isemayo “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo
Kiuchumi”, na yemelenga kutoa elimu kwa umma na hivyo kukuza uelewa
kuhusu umuhimu wa kutumia huduma rasmi za fedha ili kujikwamua kiuchumi na
kupunguza kiwango cha umasikini nchini.
Kabla
ya kutoa hotuba ya ufunguzi rasmi wa maadhimisho hayo, Waziri Mkuu alipata
fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali ili kupata maelezo ya huduma wanazotoa
na miongini mwa mabanda hayo ni banda la PSSSF, ambapo alipokelewa na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, Katibu Mkuu, Mhandisi
Cyprian Luhemeja na Mkurugenzi Mkuu, CPA. Hosea Kashimba.
Akitoa
taarifa kwa Mhe. Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba,
alisema, Mfuko pamoja na kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa wanachama na
wananchi wanofika katika banda hilo pia unatoa elimu ya fedha.
“Mhe.
Waziri Mkuu PSSSF inaingiza kwenye uchumi wa nchi kiasi cha shilingi bilioni
150 kila mwezi kama mafao ya pensheni na mafao mengine yakiwemo ya kustaafu ya mkupuo (lump sum)” Alisema.
Fedha
hizi ni nyingi, elimu inahitajika ili wanaozipokea waweze kuona namna bora ya
kutumia mafao hayo kwa maendeleo yao binafsi na uchumi wa taifa hili kwa ujumla.”
Alifafanua CPA. Kashimba.
Aidha
kuhusu ulipaji wa mafao, CPA. Kashimba alimueleza Waziri Mkuu kuwa, kwa sasa
Mfuko unalipa ndani ya siku 14 baada ya mtu kustaafu na lengo ni kwamba mtu
anapoondoka kazini akutane na cheki yake benki, alisisitiza.
Maelezo
hayo ya CPA. Kashimba yalimfanya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kusema “PSSF
mnaupiga mwingi”.
Awali
akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea mabanda ya Mifuko iliyo
chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, amewahimiza
wananchi kutembelea mabanda yaliyo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu, ikiwemo
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, PSSSF, NSSF, WCF na NHIF, ili kupata elimu ya hifadhi
ya jamii na elimu ya fedha.
“Mifuko
yetu imewekeza katika elimu ya fedha kwa umma, haiishii kulipa mafao tu,
tunatoa elimu, mfano mtu anapostaafu na kupata mafao yake tunamuwezesha kupata
elimu kabla ya kustaafu, ili mafao atakayopokea yaweze kuwa endelevu na yaweze
kumuhudumia katika kipindi chote cha maisha yake ya kustaafu.” Alifafanua
Profesa Ndalichako.
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (wapili kulia), Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Profesa Joyce
Ndalichako (wakwanza kulia), Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana
Ajira na Wenye Ulemavu), Mhandisi. Cyprian Luhemeja, (wapili kushoto),
wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba (wakwanza kushoto),
wakati akitoa taarifa ya mfuko katika Maadhimisho ya 3 ya Wiki ya Huduma ya
Fedha Kitaifa, kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Novemba 22,
2023.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Profesa Joyce Ndalichako (katikati), akionyesha alama ya “Dole” alipotembelea banda la PSSSF
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu), Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikati) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu, PSSSF, CPA. Hosea Kashimba (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge
Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Fedha, PSSSF, Bi. Beatrice Musa-Lupi (wapili kushoto), Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, PSSSF, Bw. James Mlowe na Meneja wa PSSSF, Kanda ya Kaskazini, Bi. Vones Koka, nje ya banda la PSSSF.
Afisa
Matekelezo, PSSSF, Bw. Erick Mremi (kushoto), akimpatia kijitabu cha Muongozo
wa Mwanachama, Msanii maarufu nchini, Mrisho Mpoto “Mjomba”
alipotembeela banda la PSSSF.
Afisa
Usimamizi Kumbukumbu, Hellen Mbaga
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi