Na Mwandishi wetu,Timesmajiea,Online Singida
JANA, Rais Samia Samia Suluhu Hassan, amemaliza ziara yake ya siku tatu mkoani Singira, kwa kufanya mkutano mkubwa wilaya Iramba, katika viwanja vya Shule ya Msingi Sherui.
Katika Ziara hiyo, Rais Samia, amezindua miradi mbalimbali ya maendeleo, pamoja na kutoa maelekezo mbalimbali kwa viongozi wanaomsaidia.
Rais Samia anasema Serikali itaendelea kuhakikisha huduma ya elimu inasogezwa karibu na wananachi ili kuondoa adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata elimu.
Rais Samia amesema alitoa ahadi hiyo wakati akihutubia wananchi katika eneo la uwanja wa Police Square wilayani Manyoni, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi mkoani Singida.
Rais Samia amesema kupitia mradi wa Kuimarisha Elimu ya Awali na Msingi nchini (BOOST) na Mradi wa Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP), Serikali inajenga shule za msingi na sekondari katika mikoa yote nchini.
Rais Samia anasema lengo la miradi hiyo ni kuondoa msongamano katika madarasa ili kuongeza tija na ufanisi kwenye ufundishaji kutoka wanafunzi 120 kwa darasa hadi kufikia 45.
Awali Rais Samia alifungua Shule ya Msingi Imbele yenye thamani ya sh. milioni 493.4 na mabweni ya madarasa ya Shule ya Sekondari Mwanamwema Shein katika Manispaa ya Singida.
Rais Samia pia aliweka Jiwe la Msingi, ujenzi wa barabara ya Mkiwa – Itigi – Noranga (56.9km) kwa kiwango cha lami yenye thamani ya sh. bilioni 67.2 bilioni ambayo ni sehemu ya barabara ya Makongorosi- Rungwa – Itigi – Mkiwa (413km).
Barabara hii licha ya kuunganisha ushoroba wa Tanzania na Zambia pamoja na wa kati itaunganisha pia Tanzania na ukanda wa SADC na hivyo kuchochea shughuli za uzalishaji na biashara kwa kurahisisha usafiri na usafirishaji.
Kupitia ziara hiyo, Rais Samia, amewataka viongozi mkoani Singida kuwa na mikakati ya kutumia fursa za kiuchumi badala ya
kujikita kwenye sekta moja tu ili kuongeza kasi ya maendeleo ya mkoa huo.
Akihutubia wananchi katika maadhimisho ya miaka 60 ya mkoa huo yaliyofanyika katika uwanja wa Bombadi, Rais Samia amewataka viongozi kuwahamasisha wananchi kupanda mazao yanayostahamili ukame pamoja na kutumia mbegu bora na za muda mfupi.
Rais Samia pia amewahimiza wananchi kulima mazao ya alizeti, dengu na ufuta ambayo hustawi katika maeneo mengi ya mkoa wa Singida pamoja na zao la korosho ambalo pia linafanya vizuri katika maeneo mengi ya mkoa huo.
Vile vile, Rais Samia ameiagiza Wizara ya Kilimo kuhakikisha miradi ya umwagiliaji inatekelezwa katika maeneo yote yaliyobainishwa kwa ajili ya ujenzi wa skimu.
Awali Rais Samia alizindua daraja la Msingi lenye urefu wa mita 100 lililopo Wilaya ya Mkalama ambalo limegharimu kiasi cha takribani sh. bilioni 11.2.
Akihutubia wananchi wa Mkalama Rais Samia alisema Serikali itaendelea kushughulikia changamoto za kisekta zinazoikabili wilaya hiyo hususan elimu, afya na maji.
Katika ziara hiyo, Rais Samia pamoja na mambo mengine, alipata mapokezi nakubwa, ikiwemo kutikisa ngome ya aliyekuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu, katika uchguzi wa mwaka 2020.
Akiwa mkoani Singida, Rais Samia alipokelewa na maelfu ya wananchi katika kijii anachotokea Lissu, kwenye kata ya Mahambe.
Wananchi hao waliongozwa na wazee maarufu katika kijiji hicho, akiwemo Suleiman Mohamed, Jackson Mghwai Muro (Baba Mdogo wa Lissu) na Thomas Kongoro, Baba Mkubwa wa Lissu.
Wazee hao walitangaza hadharani kumuunga mkono Rais Samia kwa kuleta maendeleo makubwa kwenye kjiji chao tangu alipoingia madarakani.
Wazee hao walikemea siasa za mfarakano na kutumia lugha za matusi na kejeli dhidi ya viongozi wa nchi, kinyume na utamaduni wa Tanzania.
Mapokezi ya Rais Samia, ameibuka kuwa tishio kubwa kwa vyama vya upinzani kuelekea uchaguzi mkuu ujao wa 2025, kutokana na umati mkubwa wa watu anaojitokeza katika ziara zake za mikoani.
Kila anapoenda kwenye ziara zake za mikoani, Rais Samia amekuwa analakiwa na umati mkubwa wa watu na kuwafanya wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini, kutabiri kuwa Rais Samia atapata ushindo mnono uchaguzi mkuu ujao wa 2025.
Kada mbalimbali za wananchi, ikiwemo madereva vijana wa bodaboda, Mama lishe, wakulima, wafugaji, wavuvi, wafanyabiashara na wananchi wa kawaida wamekuwa wanajitokeza kwa wingi kupokea Rais Samia.
Ingawa bado ni mapema na Rais Samia mwenyewe hajatangaza hadharani kuwa atagombea urais 2025, lakini Rais Samia anaonekana kuwa na ushawishi mkubwa zaidi katika vyama vyote vya siasa nchini na ni turufu kubwa kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Katika ziara zake za hivi karibuni kwenye mikoa ya kusini na sasa katikati ya Tanzania kwenye mkoa wa Singida, Rais Samia amekuwa anavutia umati mkubwa wa wananchi wenye shauku ya kumuona.
Umati mkubwa wa maelfu ya watu umekuwa ukijaza viwanja vya mipira, mikutano ya hadhara na hata barabarani Rais Samia anaposimama kuwasalimia wananchi.
Wananchi wengi wameonesha kuvutiwa na uongozi wa Rais Samia tangu aliposhika madaraka Machi 2021 baada ya kifo cha Rais John Magufuli.
Akiwa Rais wa kwanza mwanamke wa Afrika Mashariki, Rais Samia ameliongoza taifa katika kipindi cha mpito baada ya kutokea kifo cha Rais wa kwanza kufariki akiwa madarakani.
Pia, Rais Samia alishika uongozi wakati nchi imekumbwa na janga hatari la COVID-19 na akaonesha ujasiri mkubwa kukabiliana na changamoto hiyo.
Kwenye uongozi wa Rais Samia, siyo tu aliendeleza bali aliongeza kasi ya miradi yote mikubwa ya maendeleo aliyoikuta chini ya Magufuli, ikiwemo ujenzi wa reli ya SGR, ujenzi wa bwawa la umeme la JNHPP, ununuzi wa ndege za ATCL, ujenzi wa barabara, vivuko na madaraja ikiwemo daraja la Kigongo-Busisi la Mwanza.
Pamoja na yote hayo, Rais Samia ameongeza kasi ya ujenzi wa shule, zahanati, hospitali na miradi ya maji kwa kiwango kikubwa.
Rais Samia pia ameagiza Serikali yake iwekeze kwenye sekta ya Kilimo kwa kuongeza bajeti maradufu na kuvunja rekodi nchini ili kuwafikia wananchi wa chini.
Zaidi ya hayo, Rais Samia amefungua uwanja wa demokrasia, uhuru na haki nchini na kuimarisha mahusiano ya Tanzania na jumuiya ya kimataifa, pamoja na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Alipoingia tu madarakani, Rais Samia aliagiza kuwa Serikali ikamilishe majadiliano na wawekezaji wa nje ambao wanapanga kujenga kiwanda kikubwa cha kuchakata gesi asilia (LNG) mkoani Lindi, mradi ambao utaingiza uwekezaji kutoka nje wa zaidi ya shilingi trilioni 100.
More Stories
Mussa: Natamani kuendelea na masomo,nikipata shule ya bweni
Tanzania inavyowahitaji viongozi wanawake aina ya Mwakagenda kuharakisha maendeleo
SCF inavyotambua jitihada za RaisSamia mapambano dhidi ya saratani