Na Mwandishi wetu
Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amepongezwa kwa kazi nzuri anayofanya ya kuwakwamua kiuchumi watu wenye ulemavu katika eneo la Madibira Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya.Hatua hiyo imekuja kupitia Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Nyanda ya juu Kusini mwa Tanzania (REGROW).
Akizungumza Jana mkoani humo na Mkulima wa Mpunga katika Mashamba yanayopata maji kutoka kwenye mfereji wa mradi unaoboreshwa na mradi wa REGROW kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.
Sadick Chavala amesema kilimo cha uhakika wa maji kimemuinua kiuchumi kiasi cha kuwa na makazi bora, kutoa ajira kwa vijana pamoja na kusomesha watoto.
Amesema kabla ya mradi wa REGROW, maisha yake yalikuwa ni ya kusangaza lakini kwa sasa amevuna magunia zaidi ya mia moja, hali iliyomsaidia kujenga nyumba, kufungua biashara ya ushonaji iliyotoa ajira kwa wengine, Akizungumza kwa niaba ya wanakijiji cha Mkunywa kata ya Madibira Mwenyekiti wa Kijiji hicho,Angelo Mbonaga amebainisha kuwa Mradi wa REGROW umeleta maendeleo makubwa kwao na kuweza kuchangia shughuli za maendeleo ya Kijiji, pia umewawezesha kuwa na uelewa mpana wa matumizi bora ya maji kwa manufaa ya uhifadhi wa ikolojia na uhai wa Wanyamapori katika Hifadhi ya Taifa Ruaha.
Aidha Naibu Msimamizi wa Mradi wa REGROW ,Blanka Tengia amesema mradi wa kuboresha mfereji wa umwagiliaji Madibira ambao unakusudia kuwasaidia wakulima kuwa na kilimo endelevu cha umwagiliaji chenye tija na Kutumia maji kwa ufasaha kisha yaweze kutiririka na kuingia Mto Ruaha Mkuu ambao ndio tegemeo kwenye Hifadhi ya Taifa Ruaha.Shughuli ya ya kuboresha mfereji huo umegharimu takriban Shilingi 8.7 Bilioni za kitanzania na mpaka sasa umetekelezwa Kwa asilimia 49 na unatarajiwa kukamilika Januari 2024.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â