November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia: Nimefurahishwa kukamilika kwa jengo la Safina

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua rasmi Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT), katika Viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Jijini Dodoma leo

August 15, 2023.

Akizindua jengo hilo, Rais Dkt. Samia alisema amefurahishwa na kukamilika kwa jengo hilo ambalo limechukua takribani miaka sita.

“Nilikuwa kila nikipita naona mavyuma hapa kwenye hili jengo nikawa nasema litakamilika lini, toka nimelifahamu ni mavyuma tu, leo tumshukuru Mungu jengo limekamilika lakini pia limepewa jina zuri sana Safina, Safina ambayo Baba Askofu ameielezea vizuri ilimbeba Nabii Nuhu na mizigo yake yote ya wanyama na ndege”

“Nataka niwaambie kwamba ile Meli ilitua Dar es salaam na ndio maana wanyama wote wale wakaenda Serengeti , Ngorongoro na maeneo mengine na kutupa sifa Tanzania ya kuwa na wanyama wazuri na bora na Watu wanatoka Ulimwenguni kote kuja kuwaangalia, ile Meli Ilitua Dar es salaam”

“Pia jina hili linaashiria mambo makubwa kama ilivyowavusha wale, ilivushe Kanisa Anglikana lakini pia iivushe Tanzania salama, jengo hili ni la kitega uchumi kuashiri kukua kwa uchumi wa Kanisa la Anglikana, Serikali imefurahishwa kukamilika kwa mradi huu ambao utachangia kiuchumi na kijamii”

Aidha Rais Dkt. Samia aliwaagiza TRA kuendelea kukusanya Kodi kama kawaida

“Jengo hili limechukua miaka sita, huduma zitakazotolewa ndani ya jengo hili sasa tunakaribia kuzipata na nimefurahishwa kuona nembo ya NMB imetanda hapo mbele na kwamba NMB ni Wapangaji wakubwa humu ndani lakini pia TRA wapo humu ndani na mambo ya kodi yametajwa humu lakini sio kwasababu umepangishwa usamehe kodi hapana kodi yetu ikusanywe kama kawaida”

Muonekano wa Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa la Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Central Tanganyika ambalo limefunguliwa Rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu tarehe 15 Agosti, 2023.
Viongozi mbalimbali pamoja na Waumini wa Kanisa la Anglikana Tanzania wakiwa kwenye viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) kwa ajili ya Sherehe za ufunguzi wa jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo Jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) Dkt. Dickson Chilongani wakati wakiwa kwenye eneo lenye michoro ya jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo Jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) Dkt. Dickson Chilongani wakati wakiwa kwenye eneo lenye michoro ya jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo Jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) Dkt. Dickson Chilongani mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu kwa ajili ya ufunguzi Rasmi wa Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo Jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023.