Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online Manyara.
MKURUGENZI wa Kampuni ya Ngabomoa Hotel, Gaspal Ngabomoa Swai ambaye ni mmiliki wa Ngabomoa Tembo raha Hotel na Montel lodge iliyopo katika mji mdogo wa Mirerani wilaya Simanjro Mkoani Manyara amaesema anawakaribisha wadau na wafanyabishara mbalimbali ambao ni wateja wao hususani walioko ndani ya Mamlaka ya mji mdogo Mirerani na Tanzania kwa ujumla na nje ya nchi ili waje kupata huduma nzuri na yenye viwango vya kimataifa.
Pia amesema kuwa kuelekea sikukuu ya za Pasaka na Id –El Fitir wanatarajia kufanya uzinduzi mkubwa wa Klub yao ambayo ni klub ya kisasa nakwamba ameamua kufanya uwekezaji huo mkubwa kutokana na aina ya maisha ambayo alikuwa ameyaishi huko nyuma na ndio maana ameweza kufanya uwekezaji mkubwa na kwakuazia amewekeza katika ujenzi wa hotel kubwa ya kisasa ambapo ndani yake kuna klub.
Mkurugenzi Ngabomoa ameyasema haya Aprili 6 mwaka huu wakati akazingumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari ambao pia walifika hotelini hapo kwa lengo la kujionea uwekezaji huo mkubwa iliofanywa na Mtanzania mzawa, ambapo pamoja na mambo mengine ameweza kutoa ajira nyingi kwa vijana wakitanzania ambao wanaendesha maisha yao kupitia uwekezaji wake.
“Kwa kweli katika maisha yangu nilipitia changamoto kubwa sana na ndio maana nikaamua kufanya uwekezaji huu hususani hapa Mirerani na kimsingi niliamua kujiajiri mimi mwenyewe na pia niweze kuajiri watanzani wezangu na nimetoa fursa ya ajira kwa watanzania wezangu na kadri inavyokwenda nitaendelea kuajiri watanzania.
Ameongeza kuwa katika kipindi chake cha miaka miwili ya Rais Samia ameweza kurudisha hali ya mshikamano na amani na amekuwa akitetea hata wafanyabiashara kweli wataendelea kumuunga mkono ili mama aendelee kufanya vizuri katika uongozi wake na kuhusu uwekezaji yeye binafsi ameamua kuwekeza mirerani japokuwa changamoto ni nyingi lakini amemua kutafuta faida ya kinyonga ya kidogo kidogo.
Amefafanua kuwa amependa kufanya hivi kwasababu alipofika eneo hilo aliona awekeze tu katika eneo hilo kwani hakuna mahala pengine pa kuwekeza kikubwa serikali iliendelee kusaidia kwa kuweka miundimbinu mizuri ili kuleta muungano mzuri kama wanavyofanya pale kwenye mgodi wa Tanzania basi wafanye na maeneo mengine ili wageni waweze kuja kwa wingi na pindi wanapokuja wageni na wao angalau wanapata faida.
Amesema kuwa mirerani panahitaji kujengwa kwasababu ukiondoa uwepo wa mgodi, makazi ya watu ya kudumu lakini hakuna vyuo hivyo serikali waendelee kuunga mkono ili wao waendelee kuwekeza kuwekeza na kikubwa zaidi wakazi wa eneo hilo hasa wafanyabishara warudi kuwekeza kwenye eneo hilo ili kupafanya kukua kama ilivyo kwenye maeneo mengine.
“Nawaalika watanzania wote wafanyabishara, wadau, watalii kuja katika hotel yake ya Ngabomoa ili kupata huduma zote wanazohitaji kwani pana kumbi za kisasa, parking kubwa ya magari, chakula, vinywaji vyote vipo, maladhi kwa maana sehemu ya za kulala na kuelekea sikuku patakuwa na uzinduzi mkubwa wa klub lengo watu wakija wafurahia huduma.’’amesema
Kwa upande wake Meneja wa Hotel Dismas Deus Kagandiga na msaidizi wake Halima Hamza wamesema kuwa Hotel hiyo Ngabomoa inapatikana katika mtaa wa Songambele katika mji huo mdogo wa Mirerani na kuhusu huduma amesema wanatoa huduma mbalimbali kama alivyotangulia kusema mkurugenzi wao hivyo anawakaribisha watanzania wote kumuunga mkono Ngabomoa ukizingatia eneo hilo kwa muda mrefu lilikosa maeneo ya watu kupata furaha hivyo wao wanakwenda kutengeneza fursa ya wakazi wa mirerani na maoneo mengine ya karibu.
Amesema kuwa Aprili 8 mwaka huu wanatarajia kuzindua jengo na matarajio yao nikupokea wageni wa kutoka maeneo mbalimbali na katika uzinduzi huo watakuwa na wasanii wengi akiwepo Gusa kutoka jijini Dar es Salaa na kimsingi eneo hilo halikuwahi kupata wageni wengi hivyo kwa ukubwa wa eneo lao na namna walivyojipanga kila kitu kitakuwa sawa na watu watapata burudani nzuri sana
Hivyo, Halima ameongeza kwa katika hoteli hiyo inakwenda kuzindia ukumbi wa kipekee na wa kwaza kwa mji wa mirerani na wamejipanga kwa kila kitu kwani kuna una usalama wa hali ya juu kuna kamera na kila kitu, wahudumu ni warembo watakuwa wamevalia sare maalumu ambazo zitawatambulisha kama wao ni wahudumu hivyo anawakaribisha sana watanzania wote.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi