May 3, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bilionea Laizar aipa kongole Tume ya Madini

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online Manyara

MCHIMBAJI wa madini ya vito (Tanzanite) na Mfanyabiashara Maarufu wa Tanzania Bilionea Saniniu Leizar amesema kuwa kwenye sekta madini pamekuwepo na maendeleo makubwa kutokana na uongozi uliopo.

Laizar amesema kuwa kuanzia watendaji wa Mkoa yaani, afisa madini mkazi (RMO) anafanya kazi vizuri na pia wanaona juhudi kubwa za serikali zinazofanyika kwa lengo la kuinua sekta ya madini haswa madini ya vito ambayo ni madini ya kimkakati na hili limekuja kwa kipindi hiki cha miaka miwili.

Amesema kuwa hivi sasa katika kipindi cha miaka hii miwili mwamko ni mzuri sana na kuna maendeleo ambayo yanaonekana na katika upande wa Madini kwa upande wa Mirerani wameanza kuingia watu wa aina mbalimbali na wameanza kujenga soko la kuuza madini mirerani na kuna jengo kubwa linajengwa kwaajili ya shughuli ya Madini.

Bilione Leizar ameyasema haya Aprili 4 mwaka 2023 ofisini kwake katika mahojiano maalumu na waandishi wa habari waliofika ofisini kwake, ambapo pia amesema anamategemeo makubwa katika kipindi hiki cha miaka miwili kuna maendeleo mazuri na biashara zinaenda vizuri na uchimbaji unakwenda vizuri sana.

Amesema kuwa yeye kama Leizar anashukuru sana kwa uongozi wa serikali kwa kuipeleka nchi vizuri sana na kwamba inafurahisha watu wote bila kujari itikadi ya vyama vilivyopo na kwakweli kuna utaratibu mzuri sana na hasa kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupenda watu wote na kwamba nimtekelezaji na nikiongozi mzuri na hata anachokifanya ni kwa ajili ya mapenzi yake kwa watanzania .

Bilionea Leizar amesema kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni mpenda maendeleo hata anayoyafanya yanatekelezwa kwa wakati na mpaka sasa hivi hata kwenye sehemu mbalimbali za barabara hususani vijijini kuna marekebisho makubwa na katika upande washule zinajengwa nyingi na serikali na mambo mengi yamefanywa na uongozi wa serikali ya awamu ya sita na kama nilivyosema watu wamefurahia Sana na wanaupendo Sana

Amesema kuwa biashara zao zinafanyika vizuri sana na wanachimba kwa uhuru na hata kama ikitoa Madini na kupeleka sehemu ya kuhifadhia serikali hata yakikaa kwa muda mrefu yatakuwa salama hivyo wanafurahi sana uongozi wa Rais Dkt Samia kwani wamekuwa huru na usalama upo wa kutosha na hata katika upande wa wanajeshi waliopo hapa Mirerani wanafanya kazi nzuri Sana ya kuimarisha ulinzi na wao kama wachimbaji wanafurahia Sana.

“Tunaiamini serikali yetu kwani haimuonei mtu yeyote na ni makini sana na inawapenda watanzania wote  ndio hivyo rais alivyo kwani hanachama yeye uongozi wake ni wakujenga nchi na na hata siku moja wakati anasikiliza hotuba yake aliwahi kusema kama kusema tusemane kwa hoja.”amesema bilionea leizar.

Amesema kuwa anamuomba Mungu aendelea kumuongoza vizuri Rais kama anavyoendelea kumupa afya njema na hekima kwani rais anaupendo sana haingilii mtu na chama chake hivyo awamu hii ya sita ya Rais Samia ni neema ya Mungu kwani hata uchaguzi ujao watu wangemwacha tu aendelee tu kwani anafanya vizuri na sio kama anamsifia tu lakini hata huko mtaani wanamsifia na wanamsema kama ni mtu mwema na wanampenda sana na wanamuongelea vizuri sana hasa wilayani Simanjaro.