November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi wafurahia ujenzi wa Bwawa la Masaka, watoa neno kwa Bodi ya Maji iringa.

Na David John Timesmajira Online Iringa

WANANCHI wa vijiji vya Makota,Sadani na kaning’ombe ,kata ya Masaka wamesema kuwa ujenzi wa Bwawa la Masaka lilipo katika Wilaya ya iringa vijijini litanufaisha wananchi wa vijiji hivyo Kwa shughuli mbalimbali za kibinadamu.

Akizungumza Kwa niaba ya wananchi wake Leo Machi 7 mwaka huu Diwani wa kata ya Masaka Methew Nganyagwa amesema kuwa kwanza wanamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa upendo wake kwani na kuwezesha ujenzi wa Bwawa hilo chini ya Bodi ya Maji. ,Bonde la mto rufiji.

Amesema kuwa Bwawa hilo ambalo Kwa asiliamia kubwa limeshakamilika licha ya huduma nyingine lakini Kwa asilimia karibu 80 litaisaidia wananchi katika shughuli za Kilimo, mifugo,pamoja na uvuvi hususani katika vijiji vya Kaning’ombe,Makota,na Sadani.

“Ndugu zangu waandishi wa Habari hapa lazima niseme ukweli kwaniaba ya wananchi wangu Bwawa hili litafaidisha zaidi ya watu elfu 12000 kutoka katika vijiji vitatu na mbali na shughuli za mifugo,kilimo,na uvuvi lakini wananchi watapata Maji salama na safi.”amesema Diwani Nganyagwa.

Pia amesema kuwa kujengwa Kwa Bwawa hilo kinakwenda kujenga misingi imara ya nishati ya umeme nakwamba kama mabwawa hayo yalikuwa kama sehemu ya majaribio basi majaribio hayo ni sahihi kwasababu wananchi watapata faida ya uwepo wa Bwawa hilo.

Diwani Nganyagwa pia amesema Waziri wa Maji Juma Aweso anafanya kazi kubwa na kwakweli anafaa sana na watu wa Bodi ya Maji Bonde la mto rufiji wanafanya kazi kubwa na kimsingi wanafaa sana.

Kwaupande wake Mhandisi kutoka Bodi ya Maji ,Bonde la Mto rufiji iringa Geofrey Simkonda amesema kuwa Bwawa hilo la Masaka Bwawa hilo lina mita za ujazo laki 439.. na urefu wa tuta ni mita 260 ambapo Kina cha Bwawa hilo ni mita 14.

Pia amesema katika Bwawa hilo wamejenga matoleo ya Maji ambapo urefu wake ni mita 300 na upana wake ni mita 25 na ujenzi wa Bwawa hilo umechukua miezi sita na limeshakamilika Kwa asilimia mia Moja.

Mhandisi Simkonda amewaeleza waandishi wa Habari kwamba matarajio yao wao kama Bodi ya Maji Bonde la mto rufiji ni kujaza Maji Kwa miaka miwili lakini kutokana na upatikanaji wa mvua inaweza kuchukua miaka mitatu na matarajio yao nikuona watanzania hasa wa iringa vijiji wananufaika na Bwawa hilo.

Akizungumzia ulinzi wa Bwawa hilo amesema kuwa wanatengeneza Jumuiya ya watumia Maji ambapo Kuna Mwenyekiti na Katibu wake hivyo mtu yeyote atakayekatiza Maji au kufanya miundonbildomu yake kuharibika atakutana nao na watachukuliwa hatua kali.

“Ndugu zangu kama alivyosema Diwani Mathew kuwa mradi huu wa Bwawa la Masaka unakwenda kunufaisha wananchi kwenye eneo la kilimo.mifugo,pamoja na uvuvi hususani Kwa vijiji vitatu vinavyozunguka kata ya Masaka.

Nakuongeza kuwa ” Bwawa hili limegharimu Sh.Bilioni 1.7 hivyo wananchi lazima walisimamie Kwa maendeleo yao wenyewe na hatutakuwa tayari kuona au kuvumilia binadamu wachache wakiharibu miundombinu yake.