Na Heri shaaban, TimesMajira Online, Ilala
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Ilala Debora Magilimba amewataka wananchi wa Segerea Wilayani Ilala kulipa tozo ya Ulinzi watakaoshindwa wakamatwe wachukuliwe hatua.
Kamanda Debora alisema tozo ya Ulinzi ipo kisheria kila Mwananchi anatakiwa kulipa kila mwezi Ili kuwawezesha Walinzi shirikishi kuwanya kazi zao vizuri .
“Suala la Ulinzi shirikishi lipo kisheria Kila Mwananchi anatakiwa kulipa bila kutazama cheo chake Mwananchi anayegoma kulipa anatakiwa kikamtwa faini shilingi 300,000/= halmashauri ya Jiji ” alisema Debora .
Aidha aliwataka apewe Taarifa kwa maandishi wananchi wanaogomea kutoa pesa ya ulinzi Segerea na Wilaya ya Ilala kwa ujumla .
Alisema kata yenye changamoto ya kugomea kulipa tozo ya Ulinzi shirikishi. Waende wakajifunze CHANIKA zaidi ya WANANCHI 100 walikamatwa na kupelekwa katika mahakama ya Jiji .
Wakati huohuo alisema Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ndio Viongozi wa Ulinzi na Usalama wa Mtaa jukumu lao kubwa ni kuimalisha Ulinzi katika mitaa yao na kushirikiana na Wate ndaji wa Mtaa Wajumbe wa Mashina hawana Mamlaka ya kuwaribu suala la Ulinzi .
Akiwataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kufanya kazi kwa weledi kwa kuwa wameaminiwa hivyo watumie madaraka yao vizuri .
More Stories
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili