Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja ameitaka Makumbusho ya Taifa kutumia vifaa vya kisasa kuitangaza urithi wa asili na utamaduni wa Tanzania.
Ametoa agizo hilo alipotembelea banda la Makumbusho ya Taifa katika Onesho la Kimataifa la Kiswahili (SITE) yanayoendelea Mlimani City jijini Dar es Salaam na kujionea vifaa vya kisasa vya kidigital vinavyotumika katika kutoa taarifa mbalimbali za urithi wa asili na utamaduni nchini.
Aliipongeza Makumbusho ya Taifa kwa ubunifu na kutaka vifaa vya aina hiyo vitumike katika kutangaza urithi wa asili na utamaduni ikiwemo historia ya nchi.
“Nawapongeza kwa ubunifu huu, vifaa kama hivi vya kidigital vinatakiwa kutumika kuhamasisha utalii wa ndani”
Pamoja na pongezi hizo Mhe Waziri ametoa maelekezo kwa Taasisi hiyo kuendelea kutangaza utalii wa ndani hasa unaopatikana kwenye Jiji la Dar es Salaam kwa sababu Wizara ya Maliasili na Utalii inaelekeza nguvu katika kuitangaza Dar es Salaam kwa kwauli mbiu isemayo (Dar es Salaam imefinguka).
Makumbusho ya Taifa mko katika nafasi nzuri sana ya kutangaza utalii adhimu wa asili na utamaduni uliopo katika jiji la Dar es Salaam’ amesema Mhe. Masanja.
Mhe. Masanja ameelekeza Taasisi ya Makumbusho ya Taifa kuandaa onesho la historia ya wanyama na na mabadiliko yao kwa kutumia mikusanyo iliyopo ikiwemo meno ya tembo.
Amesema onesho hilo ni muhimu kwa ajili ya watalii wanaofikia Dar es Salaam kuona kabla hawajaenda kwenye mbuga za wanyama na hifadhi za Taifa zilizopo nchini Tanzania.
More Stories
Balozi Nchimbi kuongoza waombolezaji mazishi ya Kibiti leo
Dkt.Tulia,apewa tano kuwezesha wananchi
Nkasi yajipanga kukusanya mapatoÂ