January 17, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NIC yaongezea hamasa Serengeti Girls, yatoa milioni 40

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

NIC Insurance imekabidhi hundi ya shilingi milioni 40 kwa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mohamedi Mchengerwa ikiwa ni zawadi na motisha kwa wachezaji wa timu ya Serengeti Girls kufika hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya kombe la dunia nchini India.

Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NIC Insurance Ndugu Karimu Mechack akimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Insurance Dkt. Elirehema Doriye Kwenye Hafla ya Kuipongeza Timu ya Taifa ya Wasichana (Serengeti Girls).