Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online Mkurugenzi wa Ranchi ya Mbogo Pirmohamed Mulla (kushoto) akimkabidhi Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki (Mb) nyaraka ya umiliki wa ng’ombe dume aina ya boran kwa serikali, baada ya ranchi hiyo kutoa msaada kwa serikali ili ng’ombe huyo atumike kuzalisha mbegu na kupandikizwa kwa ng’ombe jike ili kuboresha mifugo nchini. Makabidhiano hayo yamefanyia katika viwanja vya John Mwakangale yanapofanyika Maonesho ya Wakulima (Nanenane) kitaifa jijini Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki (Mb) akimfanyia tathmini ng’ombe dume aina ya boran mwenye umri wa miaka mitatu ambaye ana kilogramu 624 na ana thamani ya Shilingi Milioni Sita baada ya serikali kukabidhiwa ng’ombe huyo kutoka Ranchi ya Mbogo, ambapo Waziri Ndaki amesema dhamira ya serikali ni kuhimilisha ng’ombe jike Laki tatu kwa mwaka wa fedha 2022/23, hivyo ng’ombe huyo atapelekwa katika Kituo cha Taifa cha Uhimilishaji kilichopo jijini Arusha kwa ajili ya kuzalisha mbegu. Waziri Ndaki amebainisha hayo baada ya makabidhiano ya ng’ombe huyo yaliyofanyika katika viwanja vya John Mwakangale yanapofanyika Maonesho ya Wakulima (Nanenane) kitaifa jijini Mbeya. Post Views: 587 Continue Reading Previous Makumbusho ya Taifa yaja na zao jipya la utaliiNext DCEA yawataka wananchi kutembelea kwenye banda lao kupata Elimu ya utambuzi wa dawa za kulevya More Stories Habari CCM imejipanga kushinda kwa kishindo November 23, 2024 Judith Ferdnand Habari Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa  November 23, 2024 Judith Ferdnand Habari Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi November 23, 2024 zena chitwanga
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi