Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
Imeelezwa kuwa nishati ya kupikia inachukua asilimia 60 hadi 70 ya matumizi ya nishati yote inayotumika nchini hapa.
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini (EWURA), imekuja na mkakati wa kuhamasisha matumizi ya kupikia kwa kutumia nishati ya gesi kwa sababu haiharibu mazingira,inaokoa afya na kupunguza gharama.
Hayo yamebainishwa na ,Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa George Mhina,wakati akizungumza na Timesmajira online ilipotembelea katika banda lao kwenye maonesho ya nanenane Kanda ya Ziwa Magharibi yanayoendelea viwanja vya Nyamh’ongolo wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
Ambapo ameeleza kuwa kila mtu anapika haijalishi tajiri au maskini hivyo nishati za kuni na mkaa ni hatari kwa mazingira na afya kwani vinazalisha hewa ya kabondayosaidi(carbondioxide) ambayo ni sumu na hiyo inathibitika unapokuwa umelala nyumbani na ukafunga madirisha na mlango uwezi kuamka asubuhi kwa sababu umevuta hewa hiyo.
Mhina ameeleza kuwa,Julai mwaka huu Waziri wa Nishati January Makamba alikuwa na ziara takribani siku 9 kwenye Kanda ya Ziwa,pamoja na mambo mengine alikuwa anahamasisha matumizi ya gesi ya kupikia nyumbani(LPG) kwa sababu nishati ya kupikia inachukua asilimia kubwa ya matumizi ya nishati zote.
Ameeleza kuwa gesi ni bora,salama na rafiki wa mazingira,wanatamani wafike mahali wahamasishe Watanzania waelewe na waepuke kutumia nishati ya kuni na mkaa kwenye kupikia kwani kuna watu wamepata matatizo ya macho kwa sababu ya nishati hizo.
“Inapunguza gharama kwani matumizi ya kilo 6,za mkaa sawa na kilo moja ya gesi,ukipiga hesabu utakuta mtu anayetumia mkaa wa 2000 kwa siku anajikuta anatumia 60000 kwa mwezi lakini kumbe angeweza kutumia shilingi 30,000 au chini ya hapo kama angetumia mtungi wa kilo 6 wa gesi,”ameeleza Mhina.
Sanjari na hayo Mhina ameeleza kuwa endapo gesi itakuwa haijaifadhiwa vizuri na kwa umakini inaweza kuleta madhara hivyo hatua za kuchukua ni kuwa mnunuzi anapaswa kuhakikisha muuzaji wa mitungi ya gesi za kupikia anakuwa na mizani kwa ajili ya kupima kilo za mitungi hiyo.
“Baadhi ya watu wanafanya vitendo vya uchakachuaji wa gesi kwa kuchukua mtungi wa kilo 30 na kuingiza kwenye mitungi ya kilo sita hivyo badala ya kununua gesi ya kilo sita unakuta kilo nne kwaio moja hakikisha unapoenda kununua gesi unapimiwa na muuzaji ana wajibu wa kuhakikisha anaweka mizani,”ameeleza Mhina.
Pia amewahimiza Watanzania kuhakikisha wanaangalia vizuri lakimu ya mtungi wa gesi isiwe inavuja huku akisisitiza kuwa mtungi wa gesi unapaswa kusafirishwa ukiwa wima na unapofika nyumbani wasikimbilie kuwasha gesi bali wanapaswa kusubili angalau kwa dakika tano utulie ndio uanze matumizi.
Mbali na hayo ameeleza hatua za kuchukua endapo unahisi harufu ya gesi au pengine unahisi gesi itakuwa ina vuja kwanza ni kutokuwasha taa yoyote kwani kunakuwa na muunganiko wa cheche katika swichi inaweza kusababisha kulipuka,kutofungua jokofu(friji),kutowasha kiberiti.
“Baada ya hapo fungua madirisha na milango yote hewa itoke na mtungi utakuwa hauna shida lakini ukiona hatua zote umezifanya lakini bado unahitaji msaada wasiliana na mtoa huduma wa kampuni husika wa gesi unayo tumia au wasiliana na EWURA moja kwa moja,”ameeleza Mhina.
Hata hivyo ameshauri kila nyumba kuwa na ndoo yenye mchanga ambayo atanitumia kudhibiti moto endapo itatokea kwa bahati mbaya jiko la gesi likalipuka,au kutumia blanketi na ndoo ya bati kufunika jiko au mtungi wa gesi ambao umelipuka.
“Moto chakula chake ni hewa ya oksijeni hivyo hupaswi kutumia maji kuzima unakuwa unauchochea kwa sababu maji pia ya hewa hiyo,hivyo tunashauri matumizi ya mchanga kwa sababu siyo wote wana uwezo wa kununua fire extinguisher,”ameeleza Mhina.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa