Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
Mashindano ya kombe la utalii yanaendelea kurindima katika uwanja mkongwe na wa kisasa wa Nyamagana jijini Mwanza huku timu ya Pamba FC ikishindwa kufurukuta dhidi ya wapinzani wao Jendele FC baada ya kukubali kichapo cha goli 2-0 katika mchezo uliochezea jana katika uwanja huo.
Timu ya Jendele FC ili ilipata goli la kwanzadakika kipindi cha kwanza kupitia mchezaji wake Ally Seif ambapo hadi mapumziko timu hiyo ilikuwa inaongoza kwa goli 1-0.

Hadi dakika ya 90 Jendele FC waliongeza goli la pili kwa mkwaju wa penalti kupitia mchezaji wake Alphonce Ernest.
Lengo la mashindano hayo ni kuhamisha utalii wa ndani kwa watanzania na kuzipa nafasi timu zinazoshiriki ligi daraja la kwanza na pili kupima vikosi vyao ili kuona wapi wanaweza kuboresha.

More Stories
Pre-Betika Tulia Marathon kuhamasisha mazoezi kwa jamii
“Michezo ni afya,ajira” -DC.Ngubiagai
Watanzania wang’ara Yas Kill Intenational half Marathon 2026