Na Daud Magesa,TimesMajira Online
JESHI la Polisi linachunguza kifo cha mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ye Sekondari Morning Star,Fatuma Makaranga mkazi wa Mtaa wa Ndofe wilayani Nyamagana.
Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 15 mwili wake unadaiwa kukutwa ndani ya tenki la maji nyumbani kwao baada ya kutoweka kwa siku kadhaa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro amethibitisha tukio la kifo cha mwanafunzi huyo na kwamba kabla ya kufikwa na mauti alitoweka nyumbani kwao Mei 25, mwaka huu na kutafutwa bila mafanikio.
Amesema, marehemu huyo alitoweka nyumbani baada ya kutokea mtafaruku kati yake na baba yake ambapo mwili wake uligunduka Juni 4, mwaka huu, majira ya saa 5:51 usiku katika Mtaa wa Ndofe wilayani Nyamagana,ukiwa kwenye Simtanki la maji nyumbani kwao.
“Juni 4, mwaka huu, familia hiyo ilihisi harufu mbaya ikitokea kwenye simtanki la maji la nyumbani hapo, hivyo walilazimika kulivunja ndipo wakabaini ni mwili wa Fatuma ukiwa tayari umeharibika,”amesema Muliro.
Amesema kuwa, jeshi hilo linafanya uchunguzi wa tukio la kifo cha mwanafunzi ili kufahamu mazingira na chanzo chake ingawa hakuna mtu anashikiliwa hadi sasa.
More Stories
Mbunge ahoji ukamilishwaji miundombinu Vituo vya afya
Mbogo aomba Tume kuchunguza madai ya waliokuwa wafanyakazi wa EAC
Dkt.Mabula aomba mabonde Ilemela yatumike kwa Kilimo cha umwagiliaji