Na Penina Malundo,timesmajira,Online
CHAMA cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kuchukua hatua kupunguza changamoto sugu ya uhaba wa walimu kwenye shule shikizi nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu kwenye Kata ya Mpepai Jimbo la Mbinga Mjini inayoongozwa na Diwani wa ACT Wazalendo Donatus Donatus Mbepera.
Akikagua ujenzi wa madarasa katika Shule Shikizi ya Mwamko, Ado amempongeza Diwani Mbepera kwa kusimamia vizuri miradi ya elimu, afya na maji katika Kata yake na kutoa rai kwa Serikali kuhakikisha Shule Shikizi zinapatiwa walimu zaidi ili kuwapunguzuia mzigo walimu wachache waliopo.
“Tumefarijika na jitihada zilizochukuliwa kwenye ujenzi wa madarasa lakini, bado kuna uhaba mkubwa wa walimu, Mathalani, hapa Shule Shikizi ya Mwamko, kuna Mwalimu Mmoja tu anayefundisha Wanafunzi 187. Hili tunalichukua na tutalifikisha Serikalini,” amesema Ado.
Akiwa katika Shule ya Sekondari ya Ali Mohamed Shein, Ado amesema kuwa falsafa ya Chama cha ACT Wazalendo ni “Siasa ni Maendeleo” na Chama kinaitekeleza kwa vitendo.
Ado ameendelea na ziara kwenye Majimbo yote ya Mkoa wa Ruvuma ambapo leo atafanya vikao katika Majimbo ya Mbinga Mjini na Nyasa.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi