Na Joyce Kasiki,Timesmajiraonline,Dodoma
RAIS Samia Suluhu Hassan amemsha shangwe za viongozai wa Shirikisho la umoja wa Machinga (SHIUMA) baada ya kupiga simu ya kiganjani na kuongea na machinga waliokuwa wakiendelera na mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo viongozi wa machinga yanayoendelea jijini Dodoma.
Akizungumza na viongozi hao wa SHIUMA,Rais Samia ameahidi kutoa shilingi milioni 10 kwa kila mkoa ili ziweze kusaidia shughuli za uendeshaji wa ofisi.
Hatua hiyo iliwafanya Machinga kupiga kelele za shangwe na kuimba nyimbo mbalimbali za kumsifia Rais kwa kuonyesha moyo huo wa kuwajali.
Rais Samia alitoa ahadi hiyo kupitia simu ya mkonni ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum Dkt.Dorothy Gwajima mara baada ya Naibu Katibu Mkuu wa SHIUMA Josephu Mwanakijiji kusoma risala yao iliyoeleza changamoto katika mafunzo hayo ambayo yalikuwa yakirushwa mubashara.
“Watoto wangu,kundi langu nimefuatilia mkutano wenu,nimesikia vchangamoto zenu,nashukuru Waziri kwa kuwapa ofisi katika Jengo la Serikali ,sasa kuanzia Julai Ofisi ya Rais itatoa milioni 10 kwa kila Mkoa,”alisema Rais Samia
Mwanakijiji alitumia pia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia kwa kuliona kundi la Machinga ni muhimu kwani mpaka sasa Wizara hii imekuwa kiunganishi kikubwa baija yao na Serikali.
“Pamoja na changamoto zinazotukabili,lakini Wizara hii imejitahidi kuweka mifumo mizuri ya kiutendaji ili baadae tuwe wafanyabiashara wakubwa imani yetu changamoto za Machinga zitapungua.”alisema
Akifungua mafunzo hayo Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima amewapa Machinga mbinu mpya za kisasa ili waweze kupata matokeo chanya ambayo yataleta maendeleo ya Machinga na Taifa kwa jumla.
Aidha Waziri Gwajima amewataka viongozi hao kuwaheshimu viongozi wa ngazi ya wilaya na mikoa lakini pia wafuate taratibu ili changamoto zao ziweze kutatuliwa.
“Naomba mfuate kanuni na taratibu zilizowekwa ili kuhakikisha wanafanya biashara zao kwa amani bila kubugudhiwa na vyombo vya usalama katika maeneo yenu.”alisema Dkt.Gwajima
Naye Naibu Waziriwa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mwanaidi Ali Hamis amesisitiza Wamachinga wote bchini kwenda sambamba na jitihada za Serikali ili kuleta maendeleo chanya. Awali
More Stories
Polisi yaonya vyama vya siasa
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia
Kujenga ofisi ya kisasa,akipewa ridhaa ya Uenyekiti