Na Esther Macha,Timesmajira,Online, Mbeya
WAZAZI na walezi wameombwa kuisaidia serikali kuibua vipaji vya watoto wenye ulemavu walivyopewa na Mungu ili waweze kulitumikia Taifa lao na kulitendea haki kundi hilo.
Imeelezwa kuwa wapo watoto wenye ulemavu ambao wamesimamiwa vizuri na wazazi mpaka sasa ni viongozi wa nchi ,changamoto waliyo nayo haiwafanyi kutokuwa na uwezo wa kushindwa kujifunza na kuleta tija katika nchi yao.
Ofisa Elimu kata ya Mapogoro Wilaya ya Mbarali ,Francis Makombe alidema wakati akizungumza na Times majira ofisini kwake juu ya mikakati ya kuwaibua watoto wenye ulemavu katika kata hiyo .
Makombe amesema kuwa kuna watoto wengi wenye ulemavu lakini wazazi na walezi wanashindwa kuwatendea haki kwa kudhani kuwa hawawezi kufanya chochote hivyo kukata tama na baadhi kushindwa hata kuwapeleka shule.
“Niwasihi wazazi na walezi kusaidia serikali kuibua vipaji vya watoto wenye ulemavu ili kuweza kuitendea haki nchi kwani wapo watoto wengi wenywe ulemavu wenye uwezo wa kuwa na vipaji mbali mbali lakini vinashindwa kuonekana kutokana kukosa sapoti kutoka wazazi “amesema Mratibu huyo.
Akielezea jitihada za wadau Makombe amesema kwamba kuna wadau ambao wamekuwa wakijitokeza kusaidia watoto waliopo katika katika mazingira magumu wakiwemo watoto wenye ulemavu waliopo katika kata ya Mapogoro wilayani hapa.
Hata ameeleza kuwa asasi zisizokuwa za kiserikali zimekuwa zikifanya jitihada za kupita nyumba kwa nyumba kuibua watoto wenye ulemavu katika kuisaidia serikali ili watoto waweze kupata haki ya kupata elimu
Mabadaga ipo shule ya Msingi na tuna watoto wenye ulemavu wa aina tofauti ambao wapo tisa (9)kutokana na wilaya hiyo kutokuwa na shule wanalazimika kuwachanganya na wanafunzi wengine katika shule ya msingi Katumba (2) iliyopo wilayani Rungwe mkoani mbeya ”amesema Makombe.
Eliza Lutanile ni mkazi wa Isenyela amesema jamii ya Mapogoro imekuwa na mwamko mzuri wa kuwatoa watoto wenye ulemavu kwa jamii ili waweze kupata haki yao ya kimsingi ya kupata elimu .
“Tunashukuru haya mashirika ambayo yamekuwa yakitutembelea kutupa elimu ya malezi ya watoto wetu hawa wenye ulemavu kujua haki ,kufuatia na tumegundua tuna watoto wengi wenye vipaji mbali mbali “amesema. Lutanile mkazi wa Isenyela.
Mbunge wa Jimbo la Mbarali , Francis Mtega amesema kuwa zipo jitihada mbali mbali ambazo zimekuwa zikifanywa na maofisa maendeleo ya jamii wa kata na wilaya katika kuwatambua watoto wenye ulemavu.
More Stories
Polisi yaonya vyama vya siasa
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia
Kujenga ofisi ya kisasa,akipewa ridhaa ya Uenyekiti