Na Esther Macha, TimesMajira Online, Mbeya
KATIKA kuadhimisha kilele cha wiki ya maji Jijini Mbeya Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Jijini hapa wametoa msaada wa mashuka ,200 ya wagonjwa yenye thamani ya shilingi mil.3 katika hospitali ya Igawilo ili yaweze kusaidia wagonjwa wanaolazwa .
Akikabidhi msaada huo jana wa mashuka Kaimu Mwenyekiti wa bodi ya maji usafi wa mazingira (UWSA)ambaye pia ni mjumbe wa bodi,Hilda Ngoye amesema kuwa mamlaka ya maji imekuwa mstari mbele katika kujitoa kwa jamii.
Aidha mjumbe huyo Bodi alishauri kuwepo na usafi wa mashuka kama yalivyokabidhiwa kwa kuwa na uangalizi mzuri yanapokuwa yanatumika kwa wagonjwa ikiwa ni ni pamoja na kuwasimamia wafuaji wa mashuka kuwa makini .
“Tumekabidhi mashuka haya yakiwa meupe hivyo ni vyema tukija siku moja kuwatembelea tuyakute yakiwa meupe “amesema Mjumbe huyo wa bodi.
Ngoye ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mstaafu wa`mkoa wa Kilimanjaro na Mbunge Mstaafu wa viti maalum mkoa wa Mbeya amesema kuwa sio kwamba hospitali hiyo ina uhaba wa mashuka kwa wagonjwa bali mamlaka huwa ina utaratibu wa kutoa misaada kwa jamii.
“Kuna maeneo mengi sana mfano shule ,wasiojiweza , na hospitali zingine lakini tumeona tutembelee hospitali yetu ya Igawilo na kutoa mashuka haya ,na huu ni msaada tu kwa jamii lakini serikali hii awamu ya sita imejitahidi sana kujenga majengo mazuri ,wodi na kuwa kazi ya serikali inaweza kuwa inafanyika lakini kama Taasisi pia wanajibu wa kusaidia serikali na ndo sababu wameleta msaada huyo wa mashuka “amesema
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Jijini Mbeya , Simon Bukuku amesema kuwa wamkeona watoe huo msaada kidogo ingawa kuna hospitali nyingine wakaona ni vema kusaidia wagonjwa.
Amesema kuwa wiki ya maji inafanyika kila mwaka kwa kufanya hivyio bodi ya wakurugenzi iliona vema kutoa msaada wa mashuka katika hospitali ya Igawilo .
Kwa upande wake Mganga mkuu hospitali ya Igawilo ambaye pia alimwakilisha Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya , Dkt. Jonas Lulandala ameshukuru uongozi wa mamlaka ya maji kwa jitihada zake za kuunga mkono shughuli za seriksali katika kusaidia wagonjwa wanaolazwa hospitalini hapo na kwamba wanamshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusimamia vizuri kutoa huduma za jamii.
More Stories
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili