Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Pwani
KAMISHNA msaidizi wa ardhi Mkoa wa Pwani amekabidhi mashauri yapatayo 68 katika baraza la ardhi na nyumba la Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani kwa wadaiwa sugu ambao hawataki kulipa kabisa kodi ya ardhi kwa kipindi kirefu ili waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine wenye vitendo kama hivyo vya kuikosesha serikali mapato kwa makusudi.
Akizungumza maara baada ya kukabidhi mashauri hayo Kamishna msaidizi wa ardhi Mkoa wa Pwani Lucy Kibwemera amebainisha kuwa kumekuwepo na wimbi kubwa la wadaiwa sugu wa ardhi hivyo wameamua kulivalia nuga suala hilo ambalo limeonekana kuwa ni tatizo kubwa katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha na kwamba wataendelea kuwasaka na kuwafuatilia wadaiwa wote sugu ambao hawataki kulipa kodi ya ardhi.
Kamishina huyo alibainisha kwamba jukumu kubwa la serikali ni kuhakikisha kwamba wanasimamia na kukusanya maduhuli yote ambayo yanatokana na ulipaji wa ardhi hivyo wananchi wote wanapaswa wanalipa kodi hizo za pango la ardhi ikiwa pamoja na kuzingatia sehria na taratibu zote zilizowekwa ili kuondokana na usumbufu.
“Kuna baadhi ya wananchi ambao katika Mkoa wa Pwani tayari tumewafikia na wengine wameshalipa kwa hiari yao wenyewe bila usumbufu lakini kuna baadhi yao bado wanakaidi kulipa kwa wakati na hawa kwa kweli hatuwezi kuwavumilia tutawachukulia hatua ili waweze kufikisha katika mabaraza ya aradhi na kushughulikiwa na hatua zaidi ziweze kuchukuliwa,”alifafanya Kamishina huyo.
“Tumeongozana na jopo la wataalamu mbali mbali wa aradhi ambao tumeweza kuwasilisha mashauri yapatayo 68 ya wadaiwa sugu katika halmashauri ya Kibaha na tumeyawasilisha katika baraza la aradhi na nyumba la Kibaha Mkoa wa Pwani na kwamba zoezi hili bado linaendelea kuwafuatilia wale wote ambao bado hawataki kulipia kodi ya ardhi,”
Katika hatua nyingine Kamishina huyo amesema kuwa bado kuna baadhi ya wananchi wanakiuka na kukaidi kukwepa kulipa kodi ya pango la ardhi na kwamba lengo la serikali sio kumwonea mtu na badala yake sheria itafuata mkondo wake ikiwemo mali zao zote kunadiwa pamoja na kufutia hati za miliki na kuwataka walipe kodi kwa hiari ili kuepukana na usumbufu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa baraza la ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani amebainisha kwamba kwa sasa wamejipanga kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wanasuluhisha changangamoto mbali mbali zinazohusiana na migogoro ya ardhi ili wananchi waweze kupata haki stahiki kwa wakati kuzingatia sheria na taratibu zilizopo.
Pia Mwenyekiti huyo alisema kwamba wao kama baraza wanaataka kuona wananchi ambao wanakabiliwa na migogoro mbali mbali ya ardhi wanajisuluhisha wao wenyewe kabla ya kwenda katika baraza hilo lengo ikiwa ni kuleta amani na utulivu kwa jamii na kwamba wataendelea kutoa huduma kwa kuzingatia misingi ya haki ambayo inaambatana na sheria na taratibu zote.
More Stories
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili