November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wakazi wa Kata ya Kibamba wampongeza Rais Samia

Na Mwandishi wetu, Timesmajira online

WAKAZI wa Kata ya Kibamba Mtaa wa Gogoni Manispaa ya Ubungo wamempogeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea Barabara ya rami yenye kilometa 2 kutoka Gogoni hadi kiluvya ambayo awali ilikuwa ni chagamoto kwao .

Mradi huo wa ujenzi unaosimamiwa na Wakala wa Barabara za vijijini na Mijini (TARURA) ulianza Novemba 2021 na unagharimu kiasi cha billioni 2 huku ukitarajia kukamilika kwa kipindi cha miezi sita.

Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti wakazi hao wameeleza kuwa barabara hiyo ilikiwa ni kikwazo kikubwa kwao katika kufanya Shughuli zao hivyo kwa sasa watafanya kazi vizuri baada ya Ujenzi huo kukamilika.

Juliana Jingu ambaye ni Mkazi wa Mtaa huo amesema awali barabara hiyo ilikuwa ni kikwazo na chagamoto kubwa kwao na kumpelekea kushidwa kufanya Shughuli zao hasa kipindi mvua inaponyesha.

“Tunamshukuru Rais wetu mama Samia kwa kutuletea mradi huu katika Mtaa wetu amefanya jambo la kheri kwa sasa tunaimani chagamoto ya uchakavu wa Barabara inakwenda kwisha”amesema Jingu

Kwa upande wake mfanyabishara katika Mtaa huo Faraji Nickolas amesema walipolezea kuhusu ujio wa mradi huo waliungana na Serikali katika suala nzima la kuacha nafasi ili mradi huo uweze kutekelezwa vizuri.

Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Gogoni Ally Arubaini amesema kwa sasa mradi huo unaendelea vizuri na utaweza kukamilika katika miezi iliyopangwa.

Awali Diwani wa kata ya kibamba Piter Ikamba aliwapongeza Wananchi wa Mtaa Gogoni kwa kuridhia uwepo wa ujenzi huo ambao unatekelezwa bila ya fidia yoyote

“Tunaishukuru Serikali ya awamu ya sita imekuwa ikifanya mambo mengi katika Mtaa huu awali tulikuwa na shida ya maji ambayo kwa sasa aipo na sasa mradi wa ujenzi wa Barabara”amesema Ikamba

Aidha aliwataka wakazi wa Mtaa huo kuilinda na kuitunza vyema miundombinu hiyo ya barabara ili fedha zilizotolewa zisiwe zimekwenda bure.