Na Heri Shabani,timesmajira,online
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam,Amos Makala ametoa agizo kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kuanza oparesheni Maalum ya kuwakamata wahalifu katika Mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa Amos Makala ameyasema hayo jana jijini humo,wakati wa majumuisho ya ziara yake ya utatuzi wa kero za wananchi katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo .
” Naagiza kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kuanzia leo muanze oparesheni ya kuwakamata waharifu wote ndani ya mkoa huu kero kubwa wananchi wetu wanakosa amani “amesema Makala.
Ameagiza hilo kushirikiana na Ulinzi Shirikishi katika oparesheni ya kamata vibaka ambayo inatarajia kuanza Leo(jana) rasmi.
Aidha Makala amewataka wazazi wa mkoa huo kukaa na watoto wao kuwauliza kazi wanazofanya vizuri wasije wakaingia katika mikono ya Sheria kwa ajili ya uhalifu.
Amesema katika mkoa wa Dar es Salaam uhalifu umeongezeka ukiwemo wizi wa vifaa vya magari ambapo wamiliki wanapofatilia wanakuta wanauziwa kifaa hicho hicho cha gari lake.
Katika hatua nyingine,Makala amesema katika ziara aliyoifanya ameona kumekithiri migogoro ya ardhi kutokana na wananchi kutapeliwa na wengine kuziwa mara mbili.
Amesema jumla ya kero zote alizopokea ni kesi 927 kati ya kesi hizo kesi 300 za mgogoro ya ardhi amezitatua.”Nazitaka Idara ya ardhi kuongeza kasi katika utatuaji migogoro mbalimbali ya ardhi huku akigiza Halmashauri husika kuwa wawazi katika utatuzi wa kesi hizo,”amesema
Kwa upande wake Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam Jumanne Mulilo amesema amepokea agizo la mkuu wa mkoa atatekeleza .
More Stories
Balozi Nchimbi kuongoza waombolezaji mazishi ya Kibiti leo
Dkt.Tulia,apewa tano kuwezesha wananchi
Nkasi yajipanga kukusanya mapato