Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Dar
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla anatarajiwa kuanza rasmi ziara ya kusikiliza na kutatua kero na changamoto za Wananchi wa Mkoa huo Jimbo kwa Jimbo ikiwa ni Mpango wake wa kupatia ufumbuzi kero za Wananchi.
RC Makalla amesema ziara hiyo itaanza rasmi Jumatatu ya Agosti 30, mwaka huu kwenye Jimbo la Kawe Viwanja vya Tanganyika Packers, Agosti 31 Jimbo la Kibamba, Septemba Mosi Jimbo la Segerea, Septemba 2 Jimbo la Mbagala na Septemba 3 Jimbo la Kigamboni ambapo zoezi litaanza kuanzia Saa 2 asubuhi.
Aidha RC Makalla amesema kutakuwa na jopo la wataalamu wabobezi wakiwemo Watendaji wa Serikali, Wanasheria, Kamishina wa Ardhi, Maafisa Ardhi, Jeshi la Polisi, TAKUKURU na Wadau wote wanaojihusisha na masuala ya kisheria.
Pamoja na hayo RC Makalla ametoa wito kwa Wananchi wote Wenye Migogoro kutumia Fursa hiyo kuwasilisha Malalamiko yao ili yaweze kupatiwa ufumbuzi kwa mujibu wa Sheria.
More Stories
Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Ubelgiji lafanyika Dar
CCM kuhitimisha kampeni kwa kishindo
Walimu elimu ya lazima watatakiwa kuwa wabobezi kwenye masomo wanayofundisha