Na Rose Itono,Timesmajira,Online
TIMU zaidi ya 100 za Jimbo la Lupa Wilayani Chunya Mkoani Mbeya zinashiriki mashindano ya Ligi ya Kasaka Cup na kugawiwa vifaa mbalimbali vya michezo.
Akizungumzia mashindano hayo Mbunge wa Jimbo la Lupa ambaye ndiye muandaaji wa mashindano hayo Masache Kasaka alisema mshindi wa kwanza atajinyakulia sh milioni moja
Amesema mshindi wa pili atajinyakulia sh 500,000 huku mshindi wa tatu akiambulia sh300,000 huku timu zote 193 zitakazoshiriki ligi hiyo zitagawiwa jezi.
Amesema ligi hiyo ambayo ameizindua rasmi jana itamalizika mwezi Oktoba kwa washindi kijinyakulia zawadi zao”,”Kasaka Cup’ 2021 itaziwezesha time hizo kujijengea uzoefu wa kushiriki ligi mbalimbali sambamba na kujenga miili yao kwani michezo ni afya,”amesema

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako