Na David John,TimesMajira Online
WANAFUNZI wanaosoma umeme wametakiwa kujitokeza kwenye viwanja vya Kimataifa vya Mwalimu Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa na kutembelea kwenye banda la Chuo cha Ualimu cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (MVTTC EETA MOROGORO)ili kupata elimu kuhusu umeme
Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye viwanja hivyo Frank Urio ambaye ni mhandis kutoka chuo hicho kilichopo mkoani Morogoro amesema kuwa wapo katika maonyesho hayo na wamekuja na kifaa kipya kuhusu umeme.
Amesema kuwa kuna changamoto kubwa sana kwa wanafunzi ambao wanakwenda kufanya mafunzo kwa vitendo na ndio maana kupitia maonyesho hayo wamekuja na kifaa hicho ili kuwapa elimu sahihi kwani ni teknolojia mpya na ndani yake kuna mafunzo ya aina mbili ambayo ni electronic mashine na nyingine.
“Ndugu waandishi kikubwa kupitia maonyesho haya tunawaomba wanafunzi wajitokeze kwa wingi ili waje kupata elimu stahiki kuhusu umeme na kama mnvyojua changamoto za umeme kwa hiyo tupo hapa hadi Julai 13 hivyo wajitokeze,”amesema mhandisi Urio
Ametoa wito kwa wanafuzni ambao wamesoma umeme waje ili wafundishwe kujua namna ya kuona vifaa hivyo jinsi vinavyofanya kazi ili akiwa katika maeneo yake ya kazi asikutane na changamoto kubwa.
Naye Sophia Tuka ambaye ni mkufunzi mwandamizi chuoni hapo akizungumzia kozi ambazo zinatolewa chuoni hapo hususani mwaka huu wa masomo amesema kuwa chuo hicho kinatoa kozi mbalimbali za ualimu na wanaandaa walimu wanaofundisha ufundi.
Amesema katika chuo chao wanatoa elimu ya ufundi katika ngazi ya cheti na pia wanatoa mafuzo kwa ngazi ya astashahada (Diploma) na mwezi wa tisa masomo yanaaza hivyo wanafunzi wajitokeze na kujiunga ili kuweza kupata elimu ya ufundi.
“Ndugu zangu wanahabari pia katika chuo chetu Tuna kozi ya postgraduetu ambayo imesajiliwa na TCU na tunashirikiana na nchuo kikuu huria na kimsingi tuna muhula wa mwezi wa tisa na nyingine itakuwa ya awamu ya pili “amsema Tuka.
More Stories
Ushiriki wa Samia G20 wainufaisha Tanzania
Dkt.Tulia ashiriki ibada, asisitiza waumini kushiriki uchaguzi serikali za mitaa
Polisi yaonya vyama vya siasa