November 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere chajivunia bunifu

Na Rose Itono,TimesMajira Online, Dar

UONGOZI WA Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere umesema miradi ya ubunifu iliyobuniwa na wanafunzi wake itasaidia kutatua changamoto mbalimbaki zinazoikabili jamii.

Mratibu wa mafunzo ya shahada za awali wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Dkt Samwel Lunyelele akizungumzia shughuli mbalimbali zinazofanywa na chuo hicho kwenye viwanja vya maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Barabara ya Kilwa Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Dar es Salaam jana Mratibu wa mafunzo ya Shahada za Awali chuoni hapo Dkt.Samwel Lunyelele amesema chuo kinajivunia bunifu mbalimbal za wanafunzi wake ikiwepo ya malipo ya maji kabla ya kutumia.

Dkt.Lunyelele amesema chuo kimezalisha wabunifu mbalimbali ambao watasaidia kutatua changamoto mbalimbali za kijamii

Akizungumzia ubunifu wake Jumbe Kambaya ambaye ni mwanafunzi wa chuo hicho aliyebuni mita ya maji ya malipo kabla alisema mita hiyo itamuwezesha mtumiaji kulipia maji kupitia mitandao ya simu kabla ya kutumia na kisha atapokea namba (token) kutoka kampuni husika na kisha kuingiza namba aluzotumiwa katika mita yake kwa kutuma ujumbe kwenye namba ya mita yake

Ameongeza kuwa utumiaji wa njia hiyo utapunguza malalamiko ya juu ya usomaji wa mita.

Naye Peter Mwakalesya mwanafunzi mwingine wa chuo hicho aliyebuni ubao unaofuta wenyewe amesema ubao huo utatatua tatizo la walimu kutumia nguvu nyingi na kuwapunguzia muda.

“Walimu wanatumia nguvu nyingi katika kufuta ubao na kupoteza Musa mwingi, “amesema Mwakalesya.

Amezitaja faida za ubao huo kuwa mbali na kupunguza muda pia zitawapunguzia walimu aza mbalimbali za kiafya wanazokutana nazo walimu kwa ufutaji ubao.