Na Severin Blasio,Morogoro
SINTOFAHAMU ya mazishi ya aliyekuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro, marehemu Isihaka Sengo imesababisha mganga mkuu wa manispaa hiyo, Ikaji Rashid kuwatawanya waombolezaji nyumbani kwa marehemu mpaka mwili wa mrehemu utakapofanyiwa uchunguzi wa kitabibu.
Utata huo ulijitokeza punde baada ya Mganga Mkuu Manispaa ya Morogoro, Ikaji Rashid kufika nyumbani kwa marehemu majira ya mchana jana na kuwakuta ndugu na jamaa wakijindaa kwenda kuzika kisha kuwataka kusitisha zoezi hilo na mwili kupelekwa chumba cha kuhifadhia maiti kwa uchunguzi.
Mganga huyo alisema, baada ya ofisi yake kupata taarifa kutoka hospitali aliyokuwa akitibiwa kwa mara ya mwisho kuna viashiria vya marehemu kuwa na maabukizi ya virusi vya Corona (COVID-19).
“Serikali inasitisha mazishi hadi itakapotangazwa vinginevyo na mwili unakwenda kuhifadhiwa chumba cha maiti, mwili huu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro na hapo tutachukua sampuli leo (jana) na kuzituma Dar es Salaam kwa uchunguzi,”alisema Mganga Rashid.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa