Na David John,Timesmajira,Online
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani imeweka wazi baada ya kufanikiwa kwa tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival mwaka 2021, imesema kwamba Kisarawe Ushoroba Festival 2022 litafanyika ndani ya wilaya hiyo na wadau wameridhia kwa kauli moja.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jocate Mwegelo ameweka wazi wilaya yao imejipanga kuendelea na Kisarawe Ushoroba Festival na kwa mikakati iliyopo wana uhakika mwaka 2022 kutakuwa na mambo mengi zaidi ukilinganisha na Kisarawe Ushoroba Festival 2021.
Aidha ameanza kukaribisha wadau na kuwashukuru WWF Tanzania na Vodacom Tanzania Foundation ambao wameahidi kuendelea kudhamini tamasha hilo.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi