September 20, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mobetto awashauri Wamama kutokata tamaa

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva na Mwanamitindo hapa nchini Hamisa Mobetto, amewataka Wamama kutokata tamaa katika kujitafutia riziki ili kutengeneza maisha yao ya baadaye pamoja na kufikia malengo waliojiwekea.

Akitoa ujumbe huo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram Mobetto amesema, kuna wakati Wamama ukutana na misukosuko mingi na kulazimika kukata tamaa huku akiwa ameachiwa mzigo mzito.

“Kuna wakati kwenye maisha tunaweza kukutana na Misukosuko, ikatulazimisha tuwe tofauti na yule tuliyetaka kuwa. Kwangu mimi maisha yalinifanya niwe ngangari, nipambane pale ambapo sikutegemea kama nitakuwa na nguvu hizo, nipambane pale ambapo sikutegemea kama nitakuwa na ujasiri ndani yangu. Maisha hayo hayo yakapelekea nikuwe kabla ya umri wangu.

“Bado ninaamini kwa uweza wa Mungu nitafika pale ambapo amenipangia nifike, kila njia nayopita sasa inanifunza kitu, na bado napambana niweze kufikia malengo na ndoto nilizojiwekea. Na hata wewe mwenzangu tulio kwenye Safari moja, usikate tamaa, twende na Mungu, Tutafika Salama,” amesema Mobetto.