November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Unaweza dhurika usipoangalia haya katika sanitizer

Mchunguzi wa dawa ,Gerald Sambu akionesha namna ya kupima sanitizer

Na  Aveline  Kitomary, TimesMajira Online, Dar es Salaam

MCHUNGUZI  wa dawa wa mamlaka ya dawa, vifaa tiba na Vitendanishi (TMDA) Gerald Sambu amesema ni muhimu kuangalia muda wa matumizi na usajili pale mtu anaponunua sanitizer ili kuweza kuepuka madhara yanayoweza kutokea.

Akianisha  madhara ya  kutumia sanitizer isiyokuwa na Ubora leo jijini Dar es Salaam,Sambu amesema zinaweza kusababisha kuchanika kwa ngozi na kutokuangamiza vijidudu kama ilivyokusudiwa.

“Tukianza kupima sanitaizer tunapima kwanza kama kuna kiasi cha kilevi ‘alcohol’ inayotakiwa kwasababu sanitizer inapoandaliwa  inatumika kemikali hivyo huenda kipimo cha tindikali na nyongo  (PH) ikawa juu au chini  ikaathiri ngozi.

“Kumbuka ngozi inapoathirika kwa kupaka sanitaizer inaweza kukusababisha maumivu mengine  tunahakikisha usalama wa sanitizer kuhakikisha ubora wake.

Sambu amesema kiwango cha kilevi kinachotakiwa katika sanitizer ni 60 hadi 80 ili kuwa na ubora na ufanisi wa kufanya kazi vizuri.

“Ikiwa sanitizer ina alcohol nyingi labda 90 hadi 100 inasababisha  ngozi kukauka haraka na kuchanika kwahiyo hata kama kuna bakteria au virusi anaweza asiuliwe vizuri hii inaweza kuleta maambukizi mengine  hivyo tunapima tindikali na nyongo  ili ngozi isiweze kuharibiwa”ameeleza.

Amesema pindi mtu anapopaka sanitizer mikononi inatakiwa kuchukua dakika moja kukauka

“Kitu cha kwanza unaponunua sanitizer  hakikisha imesajiliwa pia ni muhimu kuangalia   ‘expire date’ kuhakikisha ubora wa nje na unapochukua na kupaka haitakiwi kukukaa mkononi muda mrefu ikauke ndani ya dakika moja  ukikuta unapaka inanata  maana yake ina griseline nyingi haifanyi kazi yake vizuri na vijidudu havifi.

“Na pia endapo sanitizer itakauka ndani ya sekunde 10 inaweza isiwe na ufanisi katika mikono yako hivyo kiwango cha muda uliowekwa ndio sahihi,”amesema Sambu.