October 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ofisa TAKUKURU ampiga mwalimu mjamzito, CWT yatoa tamko

Na Fredy Mgunda, TimesMajira Online, Iringa

CHAMA cha Walimu (CWT),Wilaya ya Kilolo kimeazimia kutoshirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Iringa kutokana na tuhuma za afisa wake kumpiga mwalimu wa Shule ya Msingi Kitelewasi akiwa kwenye majukumu yake.

Katibu wa CWT Wilaya ya Kilolo Anthony Mang’waru

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Kilolo Mtemi Mgalula amesema kuwa wamefedheheshwa na kitendo cha ofisa huyo wa TAKUKURU kumpiga mwalimu kibao akiwa anatekeleza majukumu yake.

Amesema kuwa wameazimia kumpeleka mahakamani ofisa huyo wa TAKUKURU Mkoa wa Iringa kutokana na kuchukizwa na kitendo alichokifanya kisicho cha uungwana kwa mwalimu huyo.

Mgalula ameongeza kuwa wameanzimia kutoshirikiana kwa jambo lolote lile na TAKUKURU Mkoa wa Iringa ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo vimekuwa vikiwazalilisha walimu wawapo kazini.

“Hakuna jambo au tukio lolote ambao walimu wa wilaya ya Kilolo watashirikiana na TAKUKURU Mkoa wa Iringa hadi pale watakapojirekebisha na kuacha kuwanyanyasa walimu wawapo kazini” amesema.

Katibu wa CWT Wilaya ya Kilolo Anthony Mang’waru amesisitiza kuwa hawataendelea kutoa ushirikiano na TAKUKURU Mkoa wa Iringa hadi pale watakapokaa meza moja na kufikia muafaka na kusitisha vitendo hivyo vya kuwanyanyasa walimu.

Kamanda wa Taasisi ya Kuzia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Iringa,Domina Mkama amekiri kupigwa kwa mwalimu huyo ambaye ni mjamzito.

Kwa habari za kina zaidi soma Gazeti la Majira kesho