October 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa (UN), Prof. Kennedy Gaston, akiongoza kikao cha kwanza cha Kamati ya Hati za Utambulisho ya Baraza Kuu la Umoha wa Mataifa (UN)

Tanzania yaandika historia Umoja wa Mataifa

Na Mwandishi Maalum, TimesMajira Online.

KWA mara ya kwanza Tanzania imeteuliwa kuongoza nafasi nyeti katika Umoja wa Mataifa baada ya kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hati za Utambulisho ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York, kwa mwaka 2020/2021.

Uteuzi huo umependekezwa na ofisi ya Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kuidhinishwa kwa kauli moja wa wajumbe wote wa kamati hiyo ambayo inaundwa na nchi tisa, ikiwemo Marekani, China na Urusi.

Kimsingi kamati hiyo ina jukumu la kuzipatia hati zote za wawakilishi zitolewazo na wakuu wa nchi wanachama wa Mawaziri wa Nchi za Nje wanachama wa Umoja wa Mataifa na kujiridhisha iwapo zimetimiza vigezo na masharti kwa mujibu wa sheria za kitaifa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa.