November 26, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mtandao wa Polisi Wanawake TPF-Net wazindua siku 16 za kupinga ukatili

Na Israel Mwaisaka, Nkasi

‎JESHI la Polisi wilayani Nkasi mkoani Rukwa kupitia mtandao  wa Polisi Wanawake TPF-Net na dawati la jinsia, Watoto na makundi maalumu wamezindua siku 16 za kupinga  ukatili kwa kufanya matendo ya huruma kwa kutoa zawadi kwa wagonjwa na Kutoa elimu ya ukatili

‎Akizungumza  baada ya kufika katika kituo cha afya Nkomolo na hospitali ya wilaya Nkasi Mwenyekiti wa mtandao wa Polisi Wanawake TPF-Net  Ivona Mwanga alisema kuwa vipo vitendo vingi vya ukatili majumbani hivyo ni jukumu la Kila mmoja kuhakikisha vitendo vyote vya ukatili vinalipotiwa mahala husika.

‎Alisema kuwa licha ya kuwepo kwa jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali za kupambana na vitendo vya ukatili kupitia dawati la jinsia Wanawake na Watoto bado Kuna vitendo vingi vya ukatili vinavyotendwa  majumbani na kuwa bado Kila mmoja analo jukumu la kupinga ukatili kwa Kutoa Taarifa Polisi kwa wakati.

‎Alisema kuwa dhana ya ukatili ni Pana  hata kitendo cha Baba kutotoa matumizi katika familia yake ni ukatili,hivyo ni muhimu kwa vitendo hivyo vyote kuripotiwa Polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe haraka ili Kila mmoja aweze kuishi kwa amani na utulivu Kwa mujibu wa Sheria

‎Mkuu wa Dawati la jinsia, Wanawake na makundi maalumu Inspector Hance Mwakaliku amedai kuwa Leo ni siku ya uzinduzi  wa kupinga vitendo vya ukatili na kuwa watakua na siku 16 za  Kutoa elimu namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili hivyo upo umuhimu wa jamii kushiriki ipasavyo  katika harakati hizi za kupinga ukatili.

‎Alisema kuwa bado elimu kubwa Inahitajika kwa jamii juu ya Kuwepo kwa vitendo vya ukatili  kwani vipo baadhi ya vitendo vinafanyika katika jamii vya kikatili bila ya wao kijua.

‎Kaimu mratibu wa Polisi jamii Wilaya Nkasi Ramadhan Abeid  alidai kuwa vita hiyo dhidi ya vitendo mbalimbali vya kikatili inawezekana kwa maana Hadi Sasa  kata zote 28 wilayani Nkasi inao Polisi kata ambao wote jukumu lao utakua ni kupambana na vitendo hivyo na kuwa hilo linawezekana kutokana na Polisi kuwa na mtandao mpana Wilaya nzima.

‎Mkuu wa kituo cha Polisi Nkasi Mrakibu msaidizi wa Polisi ASP  Francis Mabisi alidai kuwa upo uwezekano mkubwa wa kuweza kuzuia vitendo vya ukatili kama Kila mmoja atalibeba suala hilo kwa uzito na kuwa Polisi wapo tayari Kutoa ushirikiano kwa jamii nzima na kuwa wao kama Polisi wanatamani kuona vitendo hivyo vinatoweka kabisa

‎Afisa maendeleo ya jamii kata ya Nkomolo Hilda Maginga  amessema kuwa wahanga wakubwa wa vitendo vya kikatili ni Wanawake hivyo wanalo jukumu la kuhakikisha wanakua mstari wa mbele katika  mapambano hayo kwa kushirikiana na Wanaume ambao wanachukizwa na vitendo vitendo vya ukatili.

‎Alisema kuwa kwa siku 16 za kupinga ukatili watazitumia vizuri kama maendeleo ya jamii kuhakikisha wanakutana na Watu wa makundi mbalimbali katika kuona elimu ya ukatili inamfikia Kila mmoja

‎Kila mwaka ifikapo Novemba 25 dunia uadhimisha siku 16 za kupinga ukatili ambapo Kila kada uwa na jambo la kufanya katika siku 16 zilizotengwa kupinga ukatili.