Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online,Tabora
ASKOFU wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Jimbo la Tabora Kati, Rev.Paul Meivukie ameomba Serikali ya Mkoa wa Tabora kuchukua hatua za haraka kudhibiti maeneo hatarishi ili kuepuka athari za mvua za El-nino nino.
Rev.Meivukie ametoa ombi hilo mbele ya Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa Tabora Ghullam Dewj,kwenye ibada maalumu ya uzinduzi wa Jimbo Jipya la Tabora Kati iliyofanyika katika Kanisa la Kitete Christian Centre.

Amesema,moja ya maeneo hayo kuwa ni Mtaa wa Kombo Masai uliopo katika Kata ya Usule ndani ya halmshauri hiyo ambapo alieleza kuwepo kwa mtaro unaomwaga maji mengi sana katika maeneo ya wananchi wakati wa mvua.
Rev.Meivukie amemwomba Mstahiki Meya ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa Benno Malisa kupokea ombi hilo na kuangalia namna ya kufanya ili mtaro huo usilete madhara makubwa punde mvua za El-nino zitakapoanza.
“Eneo hili lina mkondo mkubwa sana wa maji, hali ambayo imekuwa ikisababisha mafuriko wakati wa masika hivyo kuleta usumbufu kwa wananchi, naamini Mstahiki Meya utatusaidia kulifikisha mahali panapohusika,”ameeleza.
Amesisitiza kuwa Serikali inafanya kazi nzuri kukabiliana na changamoto zinazoikabili jamiii katika maeneo mbalimbali, hivyo anaamini hili litashughulikiwa ipasavyo kabla ya kuleta madhara kwa wananchi.
Akiongea na waandishi wa habari, Mstahiki Meya Ghullam Dewj amemshukuru Askofu Mkuu wa TAG Dkt Barnabas Mtokambali kwa kuzindua Jimbo hilo ambalo lipo katika halmshauri hiyo na baadhi ya maeneo ya Uyui.
Ameeleza kuwa wakazi wa halmashauri hiyo watanufaika kiroho na kimwili kwa kuwa miongoni mwa malengo yaliyoanishwa na Askofu mpya wa Jimbo hilo Rev.Paul Meivukie ni kujengwa kwa shule ya sekondari na hospitali ya Jimbo.




More Stories
Ilemela yakusanya bil. 4.37
Chunya kuwaburuta mahakamani wadaiwa wa mil.600
UN:Mabunge yana nafasi kubwa kuharakisha MaendeleoÂ