November 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbwana Samatta,

Kada wa CCM ‘Mo Noray’ ampongeza Samatta

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mdau wa soka hapa nchini Mohamed Noray ‘Mo Noray’, amempongeza Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania anayekipiga katika klabu ya Fenerbahçe S.K. inayoshiriki Ligi Kuu nchini Uturuki Mbwana Samatta, kwa kuitangaza Tanzania kwenye medani ya soka.

Noray ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi Tanzania Works Building Limited ambayo inakarabati Uwanja wa ndani wa Taifa unaotumika katika mchezo mpira wa kikapu, amekuwa mstari wa mbele kwenye suala zima la michezo hapa nchini.

Akizungumza na majira jana wakati wa kutoa maoni yake juu ya kumbukizi ya Baba wa Taifa hayati Mwalimi Julius Nyerere kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu Noray amesema, anamkumbuka sana Nyerere jinsi alivyoipa kipaumbele sekta ya michezo hivyo Watanzania hawana budi kumuenzi kuhusu hilo.

Noray amesema, Watanzania wapo takribani milioni 55 kulinganisha na nchi zilizotuzunguka katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, lakini Samatta ni mchezaji pekee katika karne hii ambaye amewatoa kimasomaso Watanzania kucheza Ligi ngumu barani Ulaya ikiwemo Astoni Villa ya England na Fenerbahçe S.K ya Uturuki.

“Ki ukweli nampongeza sana Samatta ametuletea sifa Taifa letu kujilikana barani Ulaya kutokana na juhudi zake binafsi alizosifanya mpaka kufikia alipo, hivyo ni vyema tukampa sapoti kwa hali na mali kuhakikisha Watanzania wapo nyuma yake,” amesema Noray.

Hata hivyo Noray amewataka wadau mbalimbali wa Soka hapa nchini kujitokeza kujenga viwanja vya soka na michezo mingine kwa wingi ili kutengeneza vipaji ambavyo vitaweza kufuata nyayo kama za Samatta.

Akizungumzia kuelekea kwenye uchaguzi utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu Noray amesema, kama hayati Malimu Nyerere alipenda sana kuhubiri amani, basi Watanzania hawana budi kwenda kupiga kura kwa amani ili kumchagua Rais ambaye atalifikisha Taifa hili katika mtazamo wa kimataifa huku akimtaja mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Magufuli ndiye chaguo sahihi.

Amewataka Watanzania kumchagua tena mgombea Urais wa chama hicho, Dkt. John Magufuli ili aweze kuleta maendeleo zaidi katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

%%%%%%%%%%%%%%%