Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
MTANGAZAJI wa redio Let’s Play, Willy Nkya amepanda tena Mlima Kilimanjaro akiwa na jukumu la kuripoti matukio kila siku akiwa katika kilele cha mlima huo.
Nkya, ambaye alipanda mlima Kilimanjaro kwa mara ya kwanza mwaka 2017 muda mfupi baada ya kumaliza chuo, alisema safari yake ya mwaka huu imekuwa ya tofauti kwa namna kadhaa.
Alipanda mlima akiwa na uzoefu zaidi na maandalizi ya kutosha ya mwili na uelewa mzuri wa namna ya kukabiliana na uchovu, baridi na mabadiliko ya hali ya hewa kadri anavyopanda.

Hata hivyo amesema, safari hii aliweza kuwasiliana na kutekeleza majukumu yake ya kikazi katika maeneo mengi ya mlima kulinganisha na miaka ya nyuma.
Akiwa katika safari hiyo, alitakiwa kurekodi na kutuma video, sauti, picha na taarifa mbalimbali kwa ajili ya matangazo ya redio na mitandao ya kijamii.
Amesema, mtandao wa Viwango wa Yas ulimwezesha kuendelea kutekeleza majukumu yake katika maeneo mengi aliyopita kuelekea kileleni, huku pia akiendelea kuwasiliana na familia na marafiki.

“Tofauti na mwaka 2017 ambapo mawasiliano yalikua ni ya shida, safari hii mambo yalikua ni tofauti, nimeweza kutuma video, picha, sauti na kuwasiliana bila matatizo na watu wangu wa karibu.
“Kupanda mlima Kilima Kilimanjaro si mchezo. Kuna wakati unahisi kabisa uko kwenye dunia nyingine. Mtandao wa viwango wa Yas ambao unapatikana vizuri kabisa katika maeneo mengi ya mlima tuliyopita umenisaidia kuendelea kutimiza majukumu ya kazi zangu bila shida.” amesema Nkya
Nkya ameendelea na safari hiyo hadi kufika Uhuru Peak, mita 5,895 kutoka usawa wa bahari, kilele cha juu zaidi barani Afrika.
Alisema, safari yake ya mwaka huu ilimpa picha tofauti na ile ya miaka tisa iliyopita, hasa kwa namna ambavyo mawasiliano yalivyorahisisha mambo mengi katika mazingira ya mlima huo wenye changamoto nyingi.
“Kwangu hii ndiyo maana ya Mtandao wa Viwango, mtandao unaokuwezesha kuendelea kufanya kile unachotaka kufanya hata ukiwa katika safari yenye changamoto. Nimepanda na Yas hadi Uhuru Peak na nimeendelea kuwasiliana na dunia,” amesema.

More Stories
Tume zaunganisha nguvu kuimarisha miradi ya maendeleo
Mkenda aitaka EAC kuongeza uwekezaji Sekta ya Elimu
EAC yaweka mkazo kubadili ahadi za elimu