August 13, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

MNH-Mloganzila kufanya kambi ya upandikizaji figo na urekebishaji wa mishipa ya kuchuja damu

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na African Feature Foundation na Global Image Care kutoka Korea Kusini, inatarajia kufanya kambi maalum ya upandikizaji wa figo na urekebishaji wa mishipa ya kuchuja damu kwa wagonjwa wenye changamoto ya figo kuanzia tarehe 15 hadi 19 Agosti 2026.

Akizungumza kuhusu maandalizi ya kambi hiyo, Dkt. Daud Katwana, Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Muhimbili-Mloganzila, amesema hospitali hiyo inatarajia kufanya upandikizaji wa figo kwa wagonjwa wanne (4), pamoja na kurekebisha mishipa ya kuchuja damu kwa zaidi ya wagonjwa 50.

Kwa mujibu wa Dkt. Katwana, kambi hiyo itatoa fursa kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo kupata huduma zinazohitajika bila kulazimika kusafiri nje ya nchi kwenda kufuata matibabu hayo.