Na Hamisi Miraji, Timesmajira Online
TAMASHA la kuifikia na kuhamasisha jamii kushiriki katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya limefana kutokana na muitikio kuwa mkubwa.
Tamasha hilo lililoandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Mulevya (DCEA), limefanyika leo kwenye viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam.
Katika Tamasha hilo Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda alikuwa mgeni rasmi ambapo amewataka wananchi kukataa matumizi na biashara ya dawa za kulevya kutoka moyoni sio mdomoni.

Aidha, ujumbe uliotolewa katika tamasha hilo umeendelea kusisitiza kuwa mapambano dhidi ya dawa za kulevya si jukumu la Serikali pekee, bali ni ajenda ya kila mmoja.
Katika tukio hilo, wananchi na waraibu wa dawa za kulevya walishiriki katika matembezi maalum ya kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

Matembezi hayo yalianzia eneo la Kwa Azizi Ally na kuelekea Viwanja vya Mwembeyanga.
Pia, Tamasha hilo lilijumuisha shughuli mbalimbali ikiwemo michezo, burudani na utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya matumizi na biashara ya dawa za kulevya.
Upande wa michezo, timu ya mpira wa miguu ya DCEA ilitoshana nguvu dhidi ya Wadau Mat & Soba, huku michezo mingine Wanawake wa DCEA walishinda goli zisizo na idadi dhidi ya wanawake wa mat na sober.

Kuvuta kamba, DCEA ilishinda katika michezo yote ya wanawake na wanaume, Magunia Mat waliwashinda sober.

More Stories
Dkt.Yonanzi ataka AFCON iwe fursa kujitangaza Kimataifa
Serikali yaimarisha maandalizi ya wanaparalimpiki Nchini
Yas yaendelea kuunga mkono Selous Marathon