Na Mwandiahi wetu,Ruvuma



NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhandisi Maryprisca Mahundi , anatarajiwa kushiriki Kongamano la Wanawake la “Mtoko wa Familia” litakalofanyika Julai 4, 2026 mkoani Ruvuma, likiwakutanisha wanawake, viongozi wa Serikali na wasanii kujadili ustawi wa familia, uwezeshaji wa wanawake na maendeleo ya jamii.
Mahundi amewasili Julai 3, 2026 katika Uwanja wa Ndege wa Songea kwa ajili ya kushiriki kongamano hilo lililoandaliwa na Rizex For Life Foundation ambapo alipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas, pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Kongamano hilo linatarajiwa kuwa jukwaa la kubadilishana uzoefu na kujadili fursa za kuimarisha ustawi wa familia, uwezeshaji wa wanawake na maendeleo ya jamii.

More Stories
Kiswahili Paris: Fursa Mpya, Dunia Yaungana Leo
Watatu mbaroni tuhuma mauaji ya bibi yao
UDSM yaongeza thamani ulanzi kupitia utafiti bunifu nchini