Na.Mwandishi wetu,Timesmajira
BENKI ya NMB imetunukiwa tuzo ya mchangiaji bora wa gawio baada ya kuikabidhi Serikali Sh96.9 bilioni, ikiwa ni utambuzi wa mchango wake katika kuongeza mapato ya Taifa na kuchochea utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Tuzo hiyo ilitolewa na Rais Samia Suluhu Hassan katika hafla iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Jumanne, Juni 30, 2026.
NMB iliwakilishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, CPA David Carol Nchimbi, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu, Ruth Zaipuna.

NMB ni miongoni mwa taasisi zilizotoa mchango mkubwa kwa Serikali kupitia gawio, kodi na malipo mengine ya kisheria. Hadi Juni 29, 2026, Serikali ilikuwa imekusanya Sh1.32 trilioni kutoka taasisi na mashirika mbalimbali, huku Sh800 bilioni—sawa na asilimia 60—ikitokana na gawio kutoka taasisi zilizopata faida.
Makusanyo hayo yameongezeka kwa Sh300 bilioni, sawa na asilimia 30, kutoka Sh1.02 trilioni zilizokusanywa Juni mwaka jana. Tuzo hiyo inaipa NMB nafasi ya kipekee miongoni mwa taasisi zinazotafsiri ukuaji wa biashara kuwa manufaa ya moja kwa moja kwa Serikali, wananchi na maendeleo ya Taifa.



More Stories
Serikali yambana mkandarasi kituo cha umeme Hale
Polisi wachunguza jeneza lililotelekezwa soko la Kabila
Mbaroni kwa tuhuma za ubakaji,uporaji