Na Zena Chitwanga,Timesmajiraonline,Dodoma
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, ametembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2026 yanayofanyika kitaifa jijini Dodoma na kupongeza juhudi za Shirika katika kusambaza na kuhamasisha matumizi ya gesi asilia nchini.
Ridhiwani ametembelea banda hilo jijini hapa lilipo katika Viwanja vya Chinangali Park leo Juni 17,2026 ambapo alisema kuwa kuongezeka kwa matumizi ya gesi asilia kutasaidia kupunguza gharama za nishati, kuongeza tija katika uzalishaji, kukuza uchumi wa wananchi na kuchangia maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Akizungumza katika maonesho hayo Mhandisi Mwandamizi kutoka Shirika hilo ,Hassan Temba amesema kuwa TPDC inaendelea kuhamasisha matumizi ya gesi asilia ili kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanapata nishati safi, nafuu na endelevu kwa maendeleo ya Taifa.
Hata hivyo katika banda hilo, Waziri Ridhiwani alipata fursa ya kujionea matumizi mbalimbali ya gesi asilia na kusisitiza wananchi kuchangamkia fursa ya kutumia nishati hiyo katika vyombo vya moto, viwanda, majumbani na shughuli nyingine za kiuchumi kutokana na kuwa salama, rafiki kwa mazingira na yenye gharama nafuu.

More Stories
Utafiti wafichua mazito sekta ya uvuvi baharini
Takwimu Rasmi kuongoza utekelezaji Dira 2050
TBS kuadhimisha miaka 50,kuzindua kitabu chake