Na Judith Ferdinand,Mwanza
WATUHUMIWA 11 wa makosa ya wizi na uharibifu wa miundombinu ya Serikali,wamekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kufuatia oparesheni iliofanywa na jeshi hilo kuanzia Juni 6,2026.
Akizungumza Juni 9,2026 mkoani hapa,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbord Mutafungwa,alisema katika oparesheni hiyo, ambayo hadi sasa inaendelea, wamefanikiwa kuwakamata watu 4 kwa tuhuma za wizi wa betri za solar zinazofungwa katika taa za barabarani.
Betri hizo ziliibwa katika maeneo ya barabara za Sabasaba–Buswelu na Pasiansi–Buzuruga wilayani Ilemela na barabara za Balewa,Pamba–Mbugani na barabara ya Isamillo wilayani Nyamagana,hivyo kusababisha taa hizo kushindwa kuendelea kutoa mwanga katika mitaa hiyo.
Mutafungwa amewataja watuhumiwa waliokamatwa kutokana na tuhuma hizo ni Zakaria Kolyo,Abduli Ramadhan, Ernest Mtiku ambaye ni dereva wa bajaji na Lenard Ezekiel.
Pia amesema,jeshi hilo linaendelea na oparesheni kuhusiana na tukio hilo na
kufanya mahojiano kwa watuhumiwa waliokamatwa, ambapo tumefanikiwa
kuwakamata watuhumiwa wengine 7 ambao ni wafanyabiashara wa vyuma chakavu jijini Mwanza.
Ambapo amesema,wafanyabiashara hao wanatuhumiwa kupokea betri hizo za solar zilizoibiwa, hivyo kuchochea wizi na uharibifu wa miundombinu hiyo ya barabara.
Watuhumiwa hao, ambao
wamekamatwa na wanaendelea kuhojiwa, ni John Kabesa,Richard Kabesa,Widson Anania,Yohana Luhechwe,Everist Katoto,Ally Tarimo, na John Emmanuel.
“Katika misako hiyo inayoendelea, tumefanikiwa kukamata betri 4 za taa za barabarani zinazotumia nishati ya jua (solar panel), mizani 5 inayotumika kupima uzito wa betri hizo zinapokuwa zimeibiwa na vifaa vingine vya kufanyia uhalifu,”amesema Mutafungwa na kuongeza:
‘Pia tumekamata bajaji moja
yenye namba za usajili MC 335 FJR, aina ya TVS, iliyokuwa ikitumiwa na wezi hao
kusafirisha betri kutoka kwenye maeneo ya matukio na kuzipeleka kwa wanunuzi.
Uchunguzi kuhusiana na tukio hilo unaendelea,”.
Hata hivyo amewataka wananchi wa Mkoa huo kuilinda miundombinu ya barabara iliopo katika maeneo yao kwani
miundombinu hiyo ni kwa faida yao na Serikali inatumia gharam kubwa huku akionya kutojihusisha na uhalifu huo na uhalifu mwingine

More Stories
REA yazindua usamabazaji majiko banifu Songwe
Mapato ya Ndani yaimarisha Bajeti ya Serikali
Salome:Ushirikiano wa wadau ni muhimu kufikia lengo la Nishati Safi ya Kupikia