May 20, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mamia  wajitokeza kumlaki Rio Ferdnand

Dar Es Salaam

NYOTA wa zamani wa Klabu ya Manchester United, Rio Gavin Ferdinand amewasili hapa nchini Tanzania Jumanne  19 Mei,2026 huku wananchi wakijitokeza kumlaki.

Mchezaji huyo (mstaafu) aliyechezea timu ya Taifa ya Uingereza na alijibebea umaarufu mkubwa alipoichezea Manchester United kwa miaka 12 akiwa Mlinzi wa Kati na Nahodha wa Timu hiyo bora nchini Uingereza ameingia  nchini kwa mwaliko wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Paul Christian Makonda.