Na Mwandishi Wetu,Dar
WITO umetolewa kwa Watanzania kudumisha amani,umoja na mshikamano pamoja na kufuata misingi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ili kuchochea maendeleo ya Taifa.
Hayo yalizungumzwa juzi jijini Dar-es-Salaam na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala Mohamed Msophe,mbele ya waandishi wa habari kwa ajili ya kuelezea mikakati na namna jumuiya hiyo wilayani humo ilivyojipanga kujijenga.
Msophe amehimiza umuhimu wa amani ambapo alisema,amani ni msingi wa maendeleo ya familia,jamii na taifa.
“Nawaomba Watanzania wezangu tudumishe amani umoja na mshikamano na upendo.Pia tuepuke migogoro tusaidiane na tujenge kesho ilio bora,”amesema Msophe na kuongeza:
“Amani ni jukumu letu sote kuilinda kwa sasa na vizazi vijavyo kwani historia ya nchi yetu ni kitovu cha amani.Amani ya nchi yetu ni lulu tuitumie vizuri kuitunza kama ilivyotunzwa na viongozi wetu waliotutangulia,”.

More Stories
ETDCO, Sonelgaz ya Algeria zaibua fursa za ushirikiano usafirishaji,usambazaji umeme
Wakala wa Vipimo washiriki NBC Marathon Dodoma
Miundombinu ya shule yatakiwa kulindwa