May 13, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Nondo aitaka Serikali kuongeza Mikopo kwa vijana

Na mwandishi wetu,Timesmajira

WENYEKITI wa Ngome ya Vijana Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo, Abdul Nondo ametoa wito kwa Serikaii ya Jamhuri ya Muungano kupitia Wizara ya Maendeleo ya Vijana kufungua dirisha jipya la mikopo ili kutoa fursa kwa kundi lingine la vijana kuomba mikopo hiyo.

Nondo amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari ambapo alifafanua kwamba kati ya Vijana wapatao 30384 walioomba mikopo wa awamu ya kwanza ni 78 tu ndio waliopewa.


Kwa mujibu wa Nondo alidai kwamba takwimu ya wanufaika 78 aliyoitoa ni tofauti na ilivyokuwa kwa Wizara husika kwani takwimu ilitolewa na Wizara ilionesha kwamba ni wanufaika 1961 kati ya 30384 ndio walipata mikopo kwa awamu ya kwanza.

Kiongozi huyo wa Ngome ya Vijana Taifa wa ACT Wazalendo, akifafanua kwanza idadi ya wanufaika 78 aliyoipata ni majina yao yaliyotajwa kwenye taarifa ya Wizara na idadi iliyoongezeka kufikia 1961 hajui imetoka wapi kwani hata yeye alioomba peke yake ingawa katika jedwali ameongezewa watu 10 ambao hajui wameingizwaje na atafanyaje kazi nao kwa kuwa hawatambui.

Nondo amesema kuwa ni vyema Wizara ingeeleza dhahili ukweli wa jambo hilo wametoka wapi ili kuondoa sintofahamu

Nondo amesema kwamba kutokana na idadi ndogo ya walipata mikopo ni vema dirisha la awamu ya pili ya waombaji mikopo litafunguliwa Ili itoe fursa Kwa vijana wajitikeze kuomba

Pia ili kufanikisha Vijana wengi kupata mikopo ni vema mambo kadhaa yakafanyiwa KAZI ikiwemo kuondoa kigezo Kwa mwombaji ambaye ni kijana lazima.awe na leseni ingali baadhi yao ndio kwanza wanaomba mikopo ili wafanye biashara.

Pia ameshauri Fedha zilizopelekwa Wizara za Kisekta ni vema zikarejeshwa katika Wizara ya Maendeleo ya Vijana ili itoe fursa kwa Vijana wengi kupata mikopo tofauti na ilivyo Sasa.

Pia amesistiza ni vema Wizara ikasema sababu za wengine kukosa mikopo ili wajisahihishe na wajitokeze kuomba kwa mara nyingine.