May 13, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Kombo ampongeza Rais wa Djibouti Guelleh kwa kuapishwa

Na Mwandishi wetu,Timesmajira

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo
amempongeza Rais wa Jamhuri ya Djibouti Ismaïl Omar Guelleh,kwa ushindi aliopata na kumtakia heri katika kuwatumikia wananchi wa Djibouti ambao wameonyesha imani kubwa kwake.

Kauli hiyo imekuja baada ya kuwasilisha Ujumbe Maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Rais wa Jamhuri ya Djibouti Guelleh leo nchini humo

Balozi Kombo amesema Tanzania na Djibouti ni nchi marafiki wa muda mrefu wenye uhusiano mzuri.

Balozi Kombo ametoa rai kwa wananchi wa Tanzania na Djibouti kuhakikisha wanauendeleza urafiki huo kwa manufaa wa wananchi wa pande zote mbili.

Rais Ismaïl Omar Guelleh amechaguliwa kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa sita mfululizo kufuatia ushindi alioupata kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Aprili 10, 2026.

Aidha, Waziri Kombo baada ya sherehe za uapisho alimkabidhi .l Rais Guelleh ujumbe maalumu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia .

Akihutubia baada ya kuapishwa, Rais Guelleh amewashukuru wananchi wa Djibout kwa imani na heshima kubwa waliyompatia na akaahidi kuboresha mifumo ya Elimu, kukuza uchumi na teknolojia, kuimarisha usalama wa kikanda na kuongeza ajira.

Rais Guelleh mwenye umri wa miaka 78, amehudumu katika nafasi hiyo kwa miaka 27 sasa akiliongoza taifa hilo dogo la Pembe ya Afrika lenye watu takribani milioni moja

Sherehe hizo za uapisho zimehudhuriwa na Wakuu wa nchi mbalimbali kutoka Ethiopia, Somalia, Sudan Kusini, Gabon na Yemen, pamoja na viongozi wengine mbalimbali waliowawakilisha wakuu wa nchi zao.