May 6, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge Arumeru Magharibi aomba Kiwanja cha Mpira jimboni

Na Mwandishi Wetu,Dodoma

MBUNGE  wa Jimbo la Arumeru Magharibi Dkt.Johannes Lukumay,amesema jimbo hilo linachangamoto ya uhaba  wa viwanja vya michezo licha ya kuwa na fursa kubwa ya michezo.

Dkt Lukumay ameeleza changamoto hiyo Mei 4,2026 Bungeni jijini Dodoma wakati akizungumza na Waziri   Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Paul Makonda ambapo amesema kwa sasa serikali inatakiwa kuona umuhimu  wa kuwekeza na kujenga Kiwanja cha kisasa katika jimbo hilo ili kuruhusu hata fursa nyingine kufunguka.

“Endapo  kutakuwa na kiwanja bora cha michezo basi fursa mbalimbali zitaibuka,”amesema 

Pamoja na hayo Dkt.Lukumay  nyota wa soka la kimataifa kutoka Ivory Cost , Didier Drogba kuona fursa ya kwenda kuwekeza Academy ya kisasa katika jimbo hilo.

Akijibu ombi hilo Waziri Makonda amesema amelichukua na analifanyiakazi huku akisema  Serikali ya awamu ya sasa imedhamiria kuhakikisha kuwa inaboresha lakini pia kujenga viwanja vingi vya michezo.